'Uwekezaji kwenye mamlaka za Serikali za mitaa ni uhakika'

*Rais Samia akutana na Mwenyekiti na Rais wa Big Win Philanthropy

NA OR- TAMISEMI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekutana na Mwenyekiti na Rais wa Big Win Philanthropy, Bi. Jamie Cooper aliyeambatana na Ujumbe wake, Waziri wa OR-, Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe leo Machi 26, 2022 jijini Dodoma.
Kikao hicho kina lengo la kuangalia fursa za Uwekezaji kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa zenye lengo la kuinua maisha ya watanzania.

Katika kikao hicho kwa pamoja wamekubaliana kuanza na fursa zilizopo katika eneo la kilimo ambalo linaajiri Vijana wengi pamoja na Wanawake kwa kuboresha uzalishaji, mnyororo wa thamani na masoko.

Wataalam wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Wizara ya Kilimo wanaendelea na kuandaa maandiko yatakayowezesha kuanza kwa utekelezaji wa maazimio ya kikao hicho.
Lengo la Ujumbe wa Big Win Philantrophy ni kusaidia katika kuibua fursa za uwekezaji kwenye jamii na kuhakikisha kuwa zinaleta manufaa kwenye hamii husika.

Post a Comment

0 Comments