Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Machi 24, 2022

*Kwacha ya Zambia (ZMK) inanunuliwa kwa shilingi 128.8 na kuuzwa kwa shilingi 129.7

NA GODFREY NNKO

DOLA ya Australia (AUD) inanunuliwa kwa shilingi 1707.05 na kuuzwa kwa shilingi 1724.6 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.1 na kuuzwa kwa shilingi 50.50.

Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.1 huku ikiuzwa kwa shilingi 362.2 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 18.9 na kuuzwa kwa shilingi 19.13.

Aidha,Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 154.3 na kuuzwa kwa shilingi 155.8 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 19.9 na kuuzwa kwa shilingi 20.15.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Machi 24, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa Shilingi 2287.05 na kuuzwa kwa Shilingi 2309.92.

Aidha,kwa mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3014.6 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3044.94 na Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2511.41 na kuuzwa kwa shilingi 2537.45.

Wakati huo huo, Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.23 na kuuzwa kwa shilingi 2.29 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.61 na kuuzwa kwa shilingi 0.64.

Kwa mujibu wa Benki Kuu, Dirham (AED) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inanunuliwa kwa shilingi 622.7 na kuuzwa kwa shilingi 628.8 huku sarafu ya Austria ya Schilling (ATS) ikununuliwa kwa shilingi 146.8 na kuuzwa kwa shilingi 148.1.

Post a Comment

0 Comments