Waziri Nchemba: Serikali itaongeza bajeti ya kilimo,mifugo na uvuvi

NA BENNY MWAIPAJA-WFM

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameahidi kuwa, Serikali katika bajeti Kuu ya Mwaka 2022/2023, itaongeza bajeti katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili sekta hizo ziweze kuchangia kipato cha wananchi na Taifa kwa ujumla.
Dkt. Nchemba ametoa ahadi hiyo jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Mashimba Ndaki, kujadili namna uwekezaji wa fedha za umma unaokusudiwa kufanywa kwenye Wizara yake unavyoweza kuongeza tija katika sekta ya mifugo na uvuvi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) (hayupo pichani), kujadili namna nyongeza ya bajeti inayotarajiwa kuongezwa katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, itakavyotumika na kuongeza tija katika sekta hiyo jijini Dodoma.

Amesema kuwa, sekta ya mifugo na uvuvi ikiwekewa miundombinu ya uhakika kwenye maeneo ya msingi yanayoweza kuonesha matokeo yanayopimika na ya haraka, inaweza kuleta mapinduzi makubwa ya kipato cha wananchi na hatimaye kuliwezesha Taifa kukuza uchumi wake.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki, kujadili namna nyongeza ya Bajeti inayotarajiwa kuongezwa katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, itakavyotumika na kuongeza tija katika sekta hiyo jijini Dodoma.

Dkt. Nchemba alitolea mfano wa uendelezaji wa ranchi za Taifa, kukuza shughuli za uvuvi kwa kuwekeza vitendea kazi vya uhakika yakiwemo maboti ya uvuvi kutaiweza nchi kuzalisha mazao ya mifugo na uvuvi kwa wingi na kuuza nje ya nchi ili kupata fedha za kigeni.

Alimshauri Waziri wa Mifugo na Uvuvi kuelekeza rasilimali fedha watakazopatiwa kwenye maeneo yenye viwanda vya kuchakata nyama na maziwa ili kuongeza mnyororo wa thamani pamoja na kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwenye viwanda hivyo.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru, akichangia hoja, wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokutana na Ujumbe wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ukiongozwa na Waziri wake Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), kujadili namna nyongeza ya bajeti inayotarajiwa kuongezwa katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, itakavyotumika ili kuongeza tija katika sekta hiyo jijini Dodoma.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru alisisitiza kuwa malengo ya kutaka kuipatia Wizara hiyo fedha nyingi zaidi ni kuonesha kuwa hivi sasa Serikali inataka kuona kuwa fedha hizo zinakuwa ni uwekezaji badala ya kuwa fedha za matumizi ya kawaida.

Alisema kuwa, sekta muhimu kama kilimo, mifugo na uvuvi zikiboreshwa, zitakuwa na matokeo makubwa na chanya kiuchumi na kijamii kwa sababu zitakuza ajira, zitaongeza wigo wa mauzo nje ya nchi na kuwaondolea wananchi umasikini wa kipato pamoja na kuiwezesha nchi kulipa deni lake la Taifa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kujadili namna nyongeza ya bajeti inayotarajiwa kuongezwa katika Wizara yake ya Mifugo na Uvuvi, itakavyotumika ili kuongeza tija katika sekta hiyo, Jijini Dodoma.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mashimba Ndaki, alieleza kuwa fedha zitakazotolewa na Serikali zitaelekezwa katika maeneo ya kuboresha shughuli za uvuvi ambapo wanatarajia kununua maboti ya uvuvi 348, kujenga mialo na masoko ya kuuzia samaki kwenye maeneo ya kimkakati.

Katika eneo la Mifugo, Mheshimiwa Mashimba alieleza kuwa nguvu zaidi zitaelekezwa kwenye maeneo ya kuboresha mifugo kupitia ranchi za taifa na makundi maalumu ya wafugaji, kuimarisha huduma za ugani na kunenepesha mifugo ili iwe na tija ambapo alisema kuwa sekta hizo mbili, kwa kuanzia, zitahitaji zaidi ya dola za Marekani milioni 105, sawa na takribani shilingi bilioni 270.
Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Justine Japhet, akichangia hoja, wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokutana na Ujumbe wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ukiongozwa na Waziri wake Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), kujadili namna nyongeza ya bajeti inayotarajiwa kuongezwa katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, itakavyotumika ili kuongeza tija katika sekta hiyo, Jijini Dodoma.
Kaimu Kamishna wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha na Mipango Bw. William Mhoja, akizungumza jambo, wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokutana na Ujumbe wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ukiongozwa na Waziri wake Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), kujadili namna nyongeza ya bajeti inayotarajiwa kuongezwa katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, itakavyotumika ili kuongeza tija katika sekta hiyo, Jijini Dodoma. Kulia ni Kaimu Kamishna wa Idara ya Mipango ya Kitaifa, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Royal Lyanga.
Ujumbe wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ukionhozwa na Waziri wake Mhe. Masimba Ndaki (kushoto) na Ujumbe wa Wizara ya Fedha na Mipango, ukiongozwa na Waziri wake Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kulia, wakiwa katika kikao cha pamoja, kujadili namna nyongeza ya bajeti inayotarajiwa kuongezwa katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, itakavyotumika ili kuongeza tija katika sekta hiyo, Jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Sekta ya Mifugo, Bw. Mbaraka Stambuli, alisema kuwa eneo lingine litakalopewa kipaumbele ni kukabiliana na magonjwa yanayoathiri mifugo ili kuiwezesha sekta hiyo kuzalisha nyama na maziwa, yanayokidhi viwango vya ubora vya kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news