WAZIRI WA ARDHI ATOA MAAGIZO KWA WATENDAJI WA SERIKALI

*Aonya wananchi wenye tabia ya kuvamia mashamba yaliyofutwa na Serikali

NA MUNIR SHEMWETA-WANMM

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula ametoa maagizo kwa watendaji wa Serikali kuhakikisha taratibu zinafuatwa katika kusimamia utekelezaji wa mambo ambayo Serikali iliyatolea maamuzi.
Waziri Dkt. Mabula amesema hayo leo Machi 26,2022 wakati wa kikao na viongozi wa Mkoa wa Morogoro ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika mkoa huo.
Aidha, ameonya wananchi wenye tabia ya kuvamia mashamba yaliyofutwa na Serikali na kusema kuwa, hawapaswi kufanya hivyo na halmashauri zinatakiwa kuhakikisha maeneo hayo yanapangiwa mpango wa matumizi ya ardhi.
"Pale ambapo serikali imefuta mashamba, mashamba hayo yanarudi kwenye mikono ya halmashauri ili mpango wa matumizi ya ardhi uweze kuandaliwa," amesema Mabula.
Timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Dkt. Angeline Mabula ipo katika ziara ya mikoa mitano kutoa mrejesho wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhususiana na ufumbuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news