Rais Samia awaapisha mabalozi wanne leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Balozi Macocha Mosha Tembele kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa (Multilateral Co-operation) Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Aprili, 2022. (Picha na Ikulu).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Mindi Hellen Kasiga kuwa Mkurugenzi wa Idara/Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi James Gillawa Bwana kuhudumu katika Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa (Multilateral Co-operation) katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Aprili, 2022.
Mabalozi walioapishwa wakila Kiapo cha Uadilifu. Kutoka kulia Balozi Macocha Mosha Tembele, Balozi Mindi Hellen Kasiga, Balozi Noel Emmanuel Kaganda, Balozi James Gillawa Bwana katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali Ikulu Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwaapisha Mabalozi 4 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments