RUWASA Tunduru:Tuna kazi moja tu, kumtua mama ndoo kichwani

NA DIRAMAKINI

WILAYA ya Tunduru mkoani Ruvuma imeendelea kutekeleza ujenzi wa miradi ya maji kupitia fedha za Ustawi wa UVIKO-19 ambazo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuondoa changamoto ya upatikanaji maji safi na salama katika wilayani humo.
Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhandisi Silvia Ndimbo akikagua bomba zilizopo kwenye mradi wa maji Daraja Mbili.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Mhandisi Silvia Ndimbo amesema kupitia miradi inayotekelezwa wanakwenda kutatua changamoto ya uhaba wa maji na hivyo kumuwezesha mwananchi kupata maji karibu na makazi yake tofauti na ilivyo sasa ambako baadhi ya vijiji wananchi wanatembea umbali mrefu kufuata maji.
Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Mhandisi Silvia Ndimbo (kushoto) akiwa na Mkandarasi wa mradi huo Mhandisi Stanley Mlelwa walipokuwa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo wa maji uliopo Kijiji cha Daraja Mbili.

Mhandisi Ndimbo anaeleza kwenye wilaya yao ya Tunduru Kuna miradi miwili inayotekelezwa kwa kutumia fedha za Ustawi ambako mradi wa kwanza upo Kijiji cha Kaza Moyo ambao umetengewa fedha sh.milioni 476.5 na mradi wa pili uko Kijiji cha Daraja Mbili ambao umetengewa fedha sh.milioni 498.3.

"Kazi ambazo zinaendelea katika mradi hii yote miwili ni uchimbaji wa mitaro,ulazaji wa mabomba na kuunganisha viungio ambao umbali wake ni kilometa 18.6, lakini umeshafikia umbali wa kilomita 16.Pia kuna ujenzi wa nyumba ya mitambo ambao umefika hatua ya umaliziaji wa mwisho.

"Shughuli nyingine inayoendelea ni ujengaji wa mnara wa mita tisa na tenki lenye uwezo wa lita 75000 ambalo ujenzi wake unaendelea, pia kuna ujenzi wa vituo saba vya kutekea maji na tayari vimeshamilika.Miradi hii itakikamilika itanufaisha wakazi wa kijiji cha daraja mbili kwa ujumla mradi utahudumia wakazi 3500.
"Mradi mwingine wa Kaza moyo wenyewe ukikamilika utanufaisha wakazi 3915 ambao wenyewe utekelezaji wake umefikia asilimia 75 na kazi katika miradi yote miwili zinafafana na zinakwenda sambamba na mkandarasi ni mmoja,"amesema.

Kuhusu utunzaji wa chanzo cha maji baada ya mradi kukamilika,Mhandisi Ndimbo amesema watawaomba wananchi kutunza mradi huo na chanzo chake cha maji.

Akizungumza hali ya upatikanaji maji katika Wilaya ya Tunduru ni asilimia 68 lakini wanaamini na kwamba katika bajeti ya fedha ya mwaka huu kuna miradi mingine itaanza kutekelezwa na itagharimu Sh.bilioni sita na hivyo kufikia asilimia 78 ya upatikanaji maji ifikapo 2025.

"Kwa kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji tunaamini Tunduru tutapunguza changamoto ya uhaba wa maji kwa kiwango kikubwa na kwa Sasa tunaendelea kutafuta vyanzo vipya vya maji kwani kwa sehemu kubwa vyanzo vyetu ni visima virefu vya maji,"amesema.
Kutokana na utekelezaji wa miradi hiyo, Mhandisi Ndimbo amesema anatoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwenye wilaya hiyo ili kutatua changamoto ya upatikanaji maji.Miradi hiyo ya maji inakwenda kumkomboa mwananchi wa Tunduru na hasa kumtua ndoo mama kichwani

Kwa upande wa vibarua ambao wanajishughulisha na shughuli za ujenzi katika miradi hiyo wameeleza kufurahishwa kwao na uamuzi wa Rais katika kuona umuhimu wa kutoa fedha ili itekelezwe hivyo nao wananufaika kwa kupata fedha kupitia kazi wanazofanya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news