Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Weather forecast April 13th,2022 starting 21:00 tonight

*MVUA BADO NI KUBWA MWAMBAO WA PWANI YA BAHARI YA HINDI KATIKA MAENEO YA LINDI, DAR ES SALAAM NA PWANI (IKIHUSISHA VISIWA VYA MAFIA), VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA

NA GODFREY NNKO

UTABIRI wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku wa leo Aprili 13,2022 unaletwa na mchambuzi Daniel Masunga kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA mikoa ya Ruvuma, Njombe, Lindi, Mtwara, Visiwa vya Unguja na Pemba, Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Pwani(visiwa vya Mafia) inatarajiwa kuwa na mawingu, mvua na ngurumo na vipindi vifupi vya jua.

Aidha, mikoa ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa, Songwe, Iringa, Mbeya, Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara inatarajiwa kuwa na mvua na ngurumo kwa maeneo machache na vipindi vya jua.

Kilimanjaro na Arusha inatarajiwa kuwa na mvua nyepesi kwa maeneo machache na jua huku Manyara, Dodoma na Singida ikitarajiwa kuwa na jua.

Aidha, upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 40 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kusini kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kusini. Na hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa.

TANZANIA WEATHER FORECAST 13/04/2022:HEAVY PRECIPITATION AT TIMES ARE EXPECTED OVER FEW AREAS OF THE COASTLINE REGIONS OF THE INDIAN OCEANWeather forecast for the next 24 hours, presented by Daniel Masunga from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news