WAELIMISHENI WANANCHI JUU YA UMUHIMU WA UHIFADHI-MHESHIWA MASANJA

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka Wakuu wa Mikoa, Wilaya na watendaji wa vijiji kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa maeneo ya hifadhi ili kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyama wakali na waharibifu.
Ameyasema hayo Aprili 9,2022 wakati wa kikao cha kupeana uelewa juu ya Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu vijiji 975 nchini katika ziara ya Mawaziri wa Kisekta kilichofanyika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Aidha, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu baadhi ya maeneo kupewa wananchi.

“Nampongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya maamuzi ya kuruhusu baadhi ya maeneo kupewa wananchi, niweke angalizo wananchi wajiandae kisaikolojia kukutana na wanyama wakali na waharibifu hasa tembo, simba, chui na wngineo,” Mhe. Masanja amesema.

Post a Comment

0 Comments