Wananchi wa Ngorongoro wapongeza ujenzi wa makazi yao Handeni

NA DIRAMAKINI

BAADHI ya wawakilishi wa wananchi walioamua kuhama kwa hiari ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwenda Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wamesema wameridhishwa na mazingira ya Kijiji cha Msomera na kuomba serikali kuboresha miundombinu iliyobakia.
Wakizungumza kijijini hapo leo Aprili 11, 2022 walipofanya ziara ya kuagua na kuangalia mazingira hayo ya Msomera wamesema,hali ya hewa ya kijiji hicho ni nzuri kwa kuishi pia mifugo,tofauti na walivyosikia awali kuwa kuna changamoto nyingi.

Mkazi wa kata ya Ngorongoro Paul Mamasita ambaye amefika kijijini hapo kama muwakilishi wa kwenda kuangalia mazingira amesema ameridhishwa na uwekwaji wa huduma muhimu kijijini hapo,hasa majengo,miundombinu ya barabara na maji.
Ameongeza kuwa taarifa za awali waliambiwa kwamba Msomera kuna magonjwa ya mifugo,mazingira sio rafiki kwa makazi na ufugaji lakini imekuwa tofauti na walivyokuta kwani majani ya malisho yapo.

"Kulikuwa na upotoshaji kwamba mazingira sio rafiki lakini tumekutana na wenzetu wa kule ambao ni wenyeji,wameahidi kutugea ushirikiano na kuhusu maradhi ya mifugo ni yale yale yaliopo Ngorongoro na yanatibika hivyo tupo tayari kuhamia hapa na hakuna changamoto mpya kwetu,"amesema Mamasita.
Aidha, kwa upande wake Emanuel Saitoti ameongeza kuwa hofu yake ilikuwa kwenye uwepo wa huduma za afya na elimu ila amekuta shule na zahanati vya awali vipo na bado serikali inajenga vingine kwenye mradi,hivyo uhakika wa huduma za kijamii upo.

"Msimamizi wa mradi ametuhakikishia kutajengwa shule mpya,kituo cha afya na miundombinu mingine na tumeona kwa macho yetu vipo baadhi,kwa hili tupo tayari kurudisha majibu na tutahamia Msomera,"amesema Emanuel.

Msimamizi msaidizi wa ujenzi wa nyumba hizo mhandisi Faudhi Seleman akizungumza na waandishi wa habari katika kijiji cha Msomera amesema,kuna nyumba zipo tayari kabisa na wananchi wanaweza kuhamia muda wowote huku,nyingine zikimaliziwa sehemu ndogondogo.
Ameongeza kuwa mradi umefikoa asilimia 85 na kati ya nyumba 103 asilimia kubwa zipo tayari kwaajili ya watu kuishi na mpaka tarehe 20 Aprili zoezi hilo la ujenzi litakamilika katika kijiji cha Msomera.
Mtaalam wa upimaji kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Ardhi Joseph Kessy ,amesema mpaka sasa wameshapima viwanja 4000 ambapo lengo ni viwanja 6000 na lengo ni wananchi wote kupata hati miliki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news