Wataalamu waendelea na kikao cha kuimarisha mpaka kati ya Tanzania na Kenya

NA MUNIR SHEMWETA-WANMM

KIKAO cha Kamati ya pamoja ya Wataalamu wa mipaka kati ya Tanzania na Kenya kimeanza leo Aprili 11, 2022 wilayani Tarime Mkoa wa Mara.
Kikao hicho cha Kamati ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili kinachotarajiwa kumalizika Aprili 15, 2022 wilayani humo na kitapokea mawasilisho ya kazi iliyofanyika na kutoa muongozo juu ya namna bora ya kutekeleza kazi iliyobaki.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Kanali Michael Mangwela akifungua kikao cha pamoja cha Wataalamu wa mipaka kati ya Tanzania na Kenya kinachoendelea wilayani Tarime leo Aprili 11, 2022. Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Hamdouny Mansoor (kulia), Mkuu wa Ujumbe kutoka Kenya Juster Nkoroi (katikati) na Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, Balozi Joseph Ungo (kushoto) wakiwa kwenye kikao cha pamoja cha wataalam wa mipaka wa Tanzania na Kenya kinachoendelea wilayani Tarime mkoani Mara leo.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho wilayani Tarime mkoani Mara leo kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Kanali Michael Mangwela amesema uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya Tanzania na Kenya ulenge kuimarisha mahusiano ya nchi hizo pamoja na kujadili changamoto za maeneo ya mipakani.

"Pamoja na kuimarishwa mipaka kati ya Tanzania na Kenya, lakini bado kuna maeneo ambayo baadhi ya wananchi kutoka kila upande wanaingia na kuendesha shughuli zao hivyo mjadili changamoto hizi kwa kina na kuja na maamuzi yatakayoleta tija," amesema Kanali Mangwela.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, Balozi Joseph Vungo akizungumza kwenye kikao cha pamoja na wataalam wa mipaka wa Tanzania na Kenya kinachoendelea wilayani Tarime mkoani Mara leo.
Ujumbe wa Tanzania na Kenya ukiwa kwenye kikao cha Pamoja cha Wataalamu wa mipaka wa nchi hizo mbili kinachoendelea wilayani Tarime leo
Mratibu Msaidizi wa Uimarishaji mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Kenya Joseph Ikorongo akiwasilisha taarifa wakati wa kikao cha pamoja cha wataalamu wa mipaka kutoka Tanzania na Kenya kinachoendelea wilayani Tarime leo.

Timu ya wataalamu wa Tanzania na Kenya imefanikiwa kukamilisha uimarishaji mpaka wa Kimataifa wa awamu ya kwanza na kuanza awamu ya pili iliyosimama kutokana na changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, Balozi Joseph Vungo amewataka wataalamu wanaoshiriki kikao hicho kuhakikisha wanajadili na kuzitolea maamuzi changamoto kwa amani hasa wakizingatia nchi ya Tanzania na Kenya zimekuwa na mahusiano mazuri.Sehemu ya washiriki kutoka Tanzania
Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Kanali Michael Mangwela akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa mipaka wa Tanzania na Kenya wakati wa kikao cha kujadili uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo mbili leo wilayani Tarime mkoani Mara. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

Kwa mujibu wa Balozi Vungo, maamuzi yoyote yatakayoamuliwa katika kikao hicho yalenge kuleta tija na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo

Zoezi la uimarishaji mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Kenya awamu ya kwanza limeanzia hifadhi ya Serengeti / Masai Mara kipande cha kilomita 60 hadi eneo la Ziwa Natron kilomita 23 na awamu ya pili inaanzia Ziwa Natron hadi Namanga eneo la Kilomita 110.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news