Waziri Aweso awazingua wataalam waliomzingua kwa taarifa 'isiyo sahihi' Handeni

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ameagiza kamanda wa jeshi la polisi wilayani Handeni mkoani Tanga,kuwakamata na kuwaweka ndani mtaalam wa mabwawa kutoka wizara hiyo kutokana na kumpa taarifa ambayo sio sahihi kuhusu ujenzi wa bwawa Kwenkambala.
Waziri Jumaa Aweso ametoa maagizo hayo leo kwenye ziara yake ya kukagua ujenzi wa bwawa la maji la Kwenkambala wilayani Handeni ambalo ujenzi umesimama na kusema kuwa wasaidizi wake wameshindwa kumpa taarifa sahihi wakati ni wajibu wao.
Walioagizwa kukamatwa na Waziri Aweso ni Hamisi Matunguru,mkandarasi Robert Lupinda na Mhandisi Amos Mtweve mthibiti ubora kutoka makao makuu kwa kushindwa kumpa taarifa sahihi kuhusu ujenzi wa bwawa la Kwenkambala.
Amesema kuwa, yeye kama waziri mwenye dhamana hatafumbia macho wataalam ambao bado wanahujumu miradi ya maji hata kama awe na nafasi kubwa.
"Niwaombe radhi viongozi na wananchi wa Handeni kwa hadha hii,niwahakikishie tunalifanyia kazi hili jambo na nitatoa majibu ni hatua gani nitachukua,"amesema Waziri Aweso.

Hata hivyo mwenyekiti halmashauri ya mji Handeni, Mussa Mkombati amemuomba Waziri Aweso kuwa, wananchi waliozungukwa na mradi huo wa maji walipwe fedha zao za fidia kwani mkandarasi ameshalipwa.

Mkombati ameongeza kuwa, walihisi tangu awali wao kama madiwani uwezo wa mkandarasi ni mdogo,ila walidharauliwa na kuambiwa wanaleta siasa kwenye jambo hilo.
Awali Katibu wa CCM wilaya ya Handeni, Anastazia Amas amemueleza Waziri Aweso kuwa walitegemea msimu huu wa mvua bwawa hilo lingekamilika,hivyo kumuomba Waziri Aweso kulifanyiakazi suala hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news