Waziri Mhagama atoa maagizo kwa TAKUKURU, ZAECA

NA JAMES K.MWANAMYOYO

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ameielekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kushirikiana na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) katika mapambano dhidi ya rushwa ili kujenga taifa lenye maadili.
Watendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Ujumbe kutoka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) uliomtembelea jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha.
Mhe. Jenista ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Watumishi wa TAKUKURU na ujumbe kutoka Mamlaka ya ZAECA ulipomtembelea ofisini kwake kujitambulisha.

Mhe. Jenista amesema ushirikiano anaoutaka uwe umejikita katika kujenga na kuimarisha utendaji kazi wa TAKUKURU na ZAECA ili kuwa na mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya rushwa.

“Ninaomba ushirikiano huo ujikite zaidi katika kubadilishana uzoefu kwenye uchunguzi wa vitendo vya rushwa, uendeshaji wa mashtaka na kuzuia vitendo vya rushwa,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Mhe. Jenista amesema ushirikiano katika kupambana na rushwa hauepukiki kwani changamoto ya vitendo vya rushwa ni suala mtambuka ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania licha ya utofauti wa sheria zinazoongoza taasisi hizi mbili za TAKUKURU na ZAECA katika mapambano dhidi ya rushwa, hivyo kuna ulazima wa kuwa na mbinu na mikakati ya pamoja itakayoliwezesha taifa kupambana na vitendo vya rushwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, Kamishna wa Polisi Ahmed Makarani akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati Watendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na ujumbe kutoka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) ulipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA, Kamishna wa Polisi, Ahmed Makarani amesema amepokea ushauri wa Mhe. Jenista wa kufanya kazi kwa ushirikiano na TAKUKURU na kuahidi kuuzingatia katika utendaji kazi wao wa kila siku ili kufanikiwa katika mapambano dhidi ya rushwa.

Ujumbe kutoka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) uko jijini Dodoma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi na TAKUKURU ili kukabiliana na vitendo vya rushwa nchini.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na Watendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na ujumbe kutoka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) uliomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bi. Neema Mwakalyelye akitambulisha ujumbe kutoka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ulipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na ujumbe wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) baada ya kuzungumza nao ulipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news