95,955 wataanza mitihani ya Kidato cha Sita kesho Mei 9,2022-NECTA

NA DIRAMAKINI

WATAHINIWA 95,955 kutoka shule za sekondari 841 na vituo vya kujitegemea 250 wanatarajia kuanza mitihani yao ya kumaliza Kidato ya Sita kesho Mei 9, 2022 na kumaliza Mei 27,2022.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dkt.Charles Msonde wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akifafanua kuwa,watahiniwa 9,670 kutoka vyuo 70 wamesajiliwa kufanya mitihani ya mwisho ya kozi ya ualimu katika ngazi ya Stashahada na cheti.

Amesema, kati ya watahiniwa wa Kidato cha Sita 85,531 ni wale wa shule na 10,424 ni wa kujitegemea.

"Kati ya hao wanaume ni 47,859 sawa na asilimia 55.96 na wasichana ni 37,672 sawa na asilimia 44.04, watahiniwa wenye mahitaji maalumu wapo 151 na kati yao 136 ni wenye uoni hafifu na 15 ni wasioona,"amefafanua.

Amesema, kati ya watahiniwa wa kujitegemea 10,424 waliojisajili, wanaume ni 6,546 sawa na asilimia 62.80 na wanawake ni 3,878 sawa ana silimia 37.20 na asiyeona ni mmoja.

Pia amesema, kati ya walimu wataketi kufanya mtihani huo, 4,560 ni ngazi ta stashahada na 5,110 ni ngazi cheti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news