BREAKING NEWS:Waziri Bashungwa amsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Masasi, Apoo Tindwa

NA FRESHA KINASA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Innocent Bashungwa, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Masasi, Apoo Tindwa kutokana na tuhum za kuhusika katika ubadhirifu wa fedha za maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime zilizokuwa zikitolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara.
Apoo Tindwa alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ambapo kuna ufujaji mkubwa wa fedha za maendeleo ikiwemo Shilingi Bilioni 5.6 za (CSR) kutoka mgodi wa Barrick North Mara.

Ambapo ameonya kuwa, kiongozi yeyote atakayefanya mchezo na fedha za serikali zinazotolewa kutekeleza miradi kwa Wananchi atachukuliwa hatua kali zaidi bila kufumbiwa macho

Waziri Bashungwa amechukua uamuzi huo leo Mei 6, 2022 wakati akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Genkuru Kata ya Nyarokoba Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara ambapo pia amekagua ujenzi wa mradi wa Kituo cha Afya Cha Genkuru kilichogharimu zaidi ya Mil.700 na kusikitishwa kutokana na Kituo hicho kutokamilika kwa wakati Jambo ambalo linawafanya Wananchi wakose huduma za afya.

Amesema, serikali haipo tayari kuona fedha inazozitoa kutekeleza miradi ya Wananchi zinatafunwa na kushindwa kuwanufaisha Wananchi hivyo amewataka Watumishi wa Serikali waliopewa dhamana ya uongozi kusimamia vyema fedha zinazotolewa zilete tija kwa wananchi.

Aidha, Waziri Bashungwa ameagiza ifikapo Juni 30, 2022 Kituo cha Afya Cha Genkuru kianze kutoa huduma huku Mkurugenzi wa Afya akitakiwa kutoa fedha za kununua mashine ya x-ray kwa ajili ya kituo hicho.

Aidha, Waziri Bashungwa, amesema dhamira ya Serikali ni kuona fedha zote zinazotolewa zinawanufaisha Wananchi huku akisema Rais Samia nia yake ni kuona Watanzania wanaendelea kuneemeka na kuondokana na changamoto mbalimbali katika maeneo yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Ally Hapi, ametoa wiki mbili kwa Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoa wa Mara (TAKUKURU) ahakikishe ndani ya wiki mbili wahusika wote waliohusika na ufujaji wa fedha za miradi ya maendeleo ukiwemk ujenzi wa Kituo cha afya cha Genkuru wanafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news