Hizi hapa nauli zote za mabasi ya mikoani, daladala katika majiji na miji nchini

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini ( LATRA) imetangaza kuanza kutumika kwa nauli mpya za mabasi na daladala badala ya Mei 14,2022 kutokana kupanda kwa bei ya mafuta.

Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabara, Johansen Kahatano alikaririwa jana akisema kuwa,watoa huduma wanapaswa kubandika nauli hizo ndani ya mabasi na katika vituo vya kukatia tiketi na wale wa daladala wabandike ubavuni karibu na mlango na kutoa tiketi zenye nauli mpya.Soma hapa>>>

Hivi karibuni, LATRA ilitangaza bei mpya za nauli za mabasi na daladala nchini ambazo zilipaswa kutumika kuanzia Mei 14,2022 lakini kutokana na kupanda kwa mafuta bei hizo zimeanza kutumika,

Nauli za mabasi yaendayo mikoani zimepanda kwa daraja la kawaida ni sh. 41.29 kwa kilomita moja kutoka sh.36.89 huku daraja la kati likipanda kwa shilingi 56.88 kutoka sh.53.22 na nauli kwa wanafunzi imebakia kuwa sh. 200 kwa daladala.
Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Gilliard Ngewe wakati akitangaza bei mpya alisema nauli za daladala kuanzia kilomita 0-10 itakuwa sh. 500 kutoka sh. 400 na kilomita 11-15 nauli itakuwa sh.550 kutoka sh. 450 na bei ya mwisho ya daladala kwa kilomita 36 hadi 40 itakuwa sh.1100 kwa daladala tu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news