Mahojiano maalum ya Mgombea Urais wa TLS Prof.Edward Hoseah, ataja mambo nane usiyoyafahamu

NA DIRAMAKINI

CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu katika nafasi ya Rais, Makamu wa Rais na Mweka Hazina.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Mei 27, mwaka huu jijini Arusha, ambapo tayari kampeni za wagombea urais zimeanza tangu Aprili 15, mwaka huu na zinatarajiwa kuhitimishwa Mei 26, mwaka huu siku ambayo pia utafanyika uchaguzi katika nafasi nyingine ikiwemo ya viongozi wa kanda. 
Profesa Edward Hoseah.

Uchaguzi huo ni kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ambao hufanyika kila baada ya mwaka mmoja.

Miongoni mwa wagombea wa nafasi ya urais ni Profesa Edward Hoseah ambaye anawania nafasi hiyo kwa awamu ya pili.
Prof. Hoseah anaomba nafasi hiyo kwa mara nyingine kwa kile anachoamini kuwa, ameweza kutekeleza vyema majukumu yake katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

"Katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wangu TLS imeweza kushauri zile sheria kandamizi kuondolewa au kurekebishwa ili kuimarisha misingi ya utoaji haki nchini kwa maslahi mapana ya wananchi na ustawi wa Taifa letu;
"Mahakama imeshapokea maagizo ya kutumia Kiswahili mahakamani kwajili ya kuwafanya watu waelewe kinachoendelea wakati wa mashauri mahakamani, hivyo tayari jopo maalum la Mawakili linaendelea kutafsiri Sheria mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili;
"Tumeweza kuishauri serikali kufungua kituo cha kimataifa hapa nchini kwajili ya utatuzi wa migogoro ya kibiashara (Tanzania International Arbitration Centre) ili kuepukana na adha ya kwenda nje kutatua migogoro kwani ni gharama kubwa;
"Uongozi wa TLS kwa kushirikiana na Serikali tumeweza kupunguza gharama za bima ya Afya kwa Mawakili kutoka Milioni 1 hadi laki Tano;
"Ndani ya Mwaka mmoja wa uongozi wangu ndani ya TLS tumejitahidi kujenga mahusiano mazuri kati ya mihimili ya kiserikali na Mawakili ambapo kwa muda mrefu watu wamekuwa wakihisi tofauti;
"Kipindi cha nyuma kulikuwa na ongezeko kubwa la Mawakili feki (vishoka) lakini kwasasa tunakwenda kudhibiti hilo kwani mnamo tarehe 22 Mwezi huu(May) kwenye mkutano wa wanasheria tunakwenda kuzindua mihuri ya moto (Digital stamps) kwajili ya kuzuia mihuri na Mawakili feki mtaani;
"TLS imekuwa ikitoa msaada wa kisheria bure kwa Wananchi ambao hawana pesa ya kupata huduma ya kisheria, ili kuwawezesha wananchi kupata haki na stahili zao,"amefafanua kwa kina Prof.Hoseah.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news