MHE.MASANJA AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA WAHIFADHI

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka wananchi kushirikiana na askari wa uhifadhi ili kutunza maeneo yaliyohifadhiwa kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Ameyasema hayo hivi karibuni katika ziara ya Mawaziri wa Kisekta ya kutatua migogoro ya ardhi katika ukumbi wa Benki Kuu mkoani Mbeya.

“Tushirikiane kwa pamoja kutunza uhifadhi ili na wenyewe ututunze,” Mhe. Masanja amesisitiza.

Amefafanua kuwa, ni vyema wananchi wakaacha dhana ya kuwachukulia askari uhifadhi kama maadui na badala yake kushirikiana nao katika uhifadhi kwa maslahi ya Taifa.

Aidha, amewataka viongozi mkoani Mbeya kushirikiana kwa karibu na askari wa uhifadhi ili kulinda maeneo yaliyohifadhiwa pamoja na kuwaelimisha wananchi kwamba askari uhifadhi sio maadui wa wananchi.

Ametaja faida za kutunza maeneo yaliyohifadhiwa kuwa ni pamoja na kuhifadhi mazingira, kutunza vyanzo vya maji na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Ameongeza kuwa, maeneo yaliyohifadhiwa yanategemeana na Sekta karibia zote akitolea mfano wa Sekta ya Maji, Sekta ya Uwekezaji na Mazingira.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news