Rais Samia alivyotembelea Banda la STAMICO katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa katika Banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' Mei 3,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel jijini Arusha. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse akimwelezea Mhe. Rais Samia kuhusu Mkaa Mbadala uliopewa jina la Rafiki Briquettes unaotengenezwa kutokana na makaa ya mawe kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe STAMICO Kiwira - Kabulo mkoani Mbeya.

Dkt. Mwasse amesema mkaa huo mbadala ni suluhisho la nishati mbadala kwa ajili kupikia ikiwa ni mkakati wa STAMICO katika kutunza mazingira na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse (kushoto) akimwelezea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusu Mkaa Mbadala uliopewa jina la Rafiki Briquettes unaotengenezwa kutokana na makaa ya mawe kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe STAMICO Kiwira - Kabulo mkoani Mbeya.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse (kushoto) akimwelezea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusu Mkaa Mbadala uliopewa jina la Rafiki Briquettes unaotengenezwa kutokana na makaa ya mawe kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe STAMICO Kiwira - Kabulo mkoani Mbeya.

"Tumeshiriki kwenye maadhimisho haya ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani tukiamini kuwa hili ni jukwaa kuu na sahihi la waandishi wa habari ili bidhaa hii iingie sokoni haraka na waandishi wa habari wawe mabalozi wa kuelimisha jamii na kutangaza Nishati hii mbadala,"amesema Dkt.Mwasse.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news