'Taarifa za mfumo wa Anwani za Makazi, kutumika kwenye mawasiliano'

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu,Kaspar Mmuya ameshauri watendaji kuanza kutumia taarifa za mfumo wa Anwani za makazi Postikodi kwenye barua za ofisi ili kurahisha mawasiliano kwa watu kujua eneo zinapopatikana ofisi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu,Kaspar Mmuya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi,Optuna Kitanda na watendaji wakitazama vibao vya nyumba vilivyoandaliwa tayari kwa kubandikwa kwenye nyumba katika ziara yake kata ya Tumbi Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Pwani.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya akizungumza na watendaji (ambao hawapo kwenye picha) katika Ofisi ya Mtendaji, Kata Matumbi kukagua utekelezaji wa operesheni ya Anwani za makazi Halmashauri ya Mji wa Kibaha.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu,Kaspar Mmuya akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mji, mara baada ya kukagua utekelezaji wa Operesheni Anwani za Makazi katika Halmashauri ya Mji huo.

“Watendaji tuanze kujitambulisha kwenye mikutano kwa mfumo wa Anwani za makazi ili kutoa hamasa zaidi kwa wananchi alisema Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu,”amesema.

Naibu Katibu Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu ametoa ushauri huo leo tarehe 19/05/2022 Katika ziara yake ya kikazi Mkoani Pwani Halmashauri ya Kibaha Mji, alipoenda kujionea utekelezaji wa Operesheni Anwani za makazi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu,Kaspar Mmuya akisalimiana na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mkoani Kibaha Bwn Jakson Mwakalima katika kukagua utekelezaji wa operesheni ya Anwani za makazi Halmashauri ya Mji kibaha Mkoa wa Pwani.

Afisa Mtendaji mtaa wa mkoani A Kibaha, Bw.Jakson Mwakalima amesema tayari wameshapata mtengenezaji wa vibao vya nyumba, ambavyo mwananchi anaenda kununua kwa shilingi elfu Mbili na kubandika kwenye nyumba yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news