Tunaiomba Serikali iendelee na mafunzo ya MEWAKA-Walimu

NA ASILA TWAHA,OR-TAMISEMI

WASHIRIKI wa Mafunzo Endelevu Kazini (MEWAKA) wameiomba Serikali kuendelea kuvisimamia na kuviwezesha vituo vya MEWAKA katika shule ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi na kwa kupitia vituo hivyo walimu waeleze changamoto zao.
Hayo yamebainishwa na mshiriki wa mfunzo ya MEWAKA, Mwalimu Furaha Mwakasembe katika mafunzo yaliyofanyika hivi karibuni mkoani Tabora katika Shule ya Msingi Ushokola iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, lengo la mfunzo hayo likiwa ni kuwajengea uwezo walimu.

Mwakasembe amesema, pamoja na kuchelewa kwa mafunzo hayo wanaishukuru Serikali kuona ni muhimu walimu kupatiwa mafunzo kwa lengo la kuwajengea uwezo na jinsi ya kuviendeleza vituo vya MEWAKA shuleni.

Aidha, amesema walimu itawasaidia kujifunza, kutatua changamoto na kupata maarifa mapya wanapokutana watabadilisha uzoefu na kushauriana sababu kazi ya ualimu kila siku unatakiwa uwe ana mbinu mpya za ujifunzaji na ufundishaji.
Hata hivyo, pamoja na mafunzo hayo kuendelea ambapo kila shule imepata nafasi ya ushiriki wa walimu wawili mwalimu wa taaluma na mwalimu mahiri amesema wakimaliza mafunzo hayo wanaenda kuwa mfano na viongozi bora kwa walimu wenzao kuweza kushirikiana nao kwa yale walio fundishwa na kwa wanafunzi wao.

“Tunaiomba Serikali kuendelea kuviwezesha na kuvipa nguvu vituo vya MEWAKA katika suala la usimamizi wa kufuata sheria, taratibu na miongozo ili visije vikasimamishwa,"amesema.

"Ili Serikali ipate maendeleo katika uboreshaji wa elimu nchini ni lazima vituo hivyo kuvisimamia sababu vitawasaidia kujua changamoto za elimu nchini” amesema Mwakasembe.
Aidha, ameiomba Serikali kuendelea kuisimamia sekta ya elimu kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu ikiwa wao walimu wa shule za awali na msingi ndio msingi elimu wapo tayari kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi waliopewa jukumu la kuwasimamia.

Naye Mwalimu Levina Mwanchang’a mshiriki wa mafunzo kutoka Shule ya Msingi Senga amesema, mwanzo walikuwa wanafundisha kwa uzoefu mwalimu hana mbinu mpya za kufundishia bila kujua kuna mabadilko katika ujifunzaji na ufundishaji kwa kupata mafunzo hayo yanaenda kuwasaidia kuongeza ujuzi na maarifa.
“Sio lazima uwe na nakala ngumu ndio uweze kupata materials unaweza kupata mbinu za kufundishia hata ukiwa na simu janja yenye uwezo wa kupata mtandao kuweza kupakua vitabu mbalimbali kutoka kwenye taasisi zetu za elimu na kupata “materials” yote haya tumeyapata kwenye mafunzo ya MEWAKA,” amesema Mwalimu Mwanchang’a.

Kwa upande wa Mratibu wa Halmashuri ya Wilaya ya Kaliua, Mwalimu Matuna Massati amesema, jumla ya washirki 226 wameshiriki na tathmini wanayoendelea kuifanya baada ya mafunzo imeonyesha walimu wapo makini.

Kwa sababu lengo la mafunzo hayo yanayoendelea ni kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao, Serikali inaamini kumalizika kwa mafunzo hayo walimu wataenda kuwa viongozi bora katika utekelezaji wa kazi zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news