Waziri Prof.Mkenda ateta na ujumbe kutoka UNICEF

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) Mei 6, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa ya Kuhudumia Watoto (UNICEF) Ofisi ya Tanzania, Dkt. Daniel Baheta.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (katikati) akizungumza na Mkuu wa Idara ya Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) ofisi ya Tanzania, Dkt. Daniel Baheta (Kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Sekta ya Elimu UNESCO Tanzania, Faith Shayo walipokutana katika ofisi za Wizara jijini Dodoma kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu mageuzi ya elimu nchini.(Picha na Wizara ya Elimu).

Sambamba na Mkuu wa Sekta ya Elimu UNESCO kwa upande wa Tanzania, Faith Shayo kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu elimu kuelekea Mkutano wa Kimataifa wa Elimu utakaofanyika mwezi Septemba 2022 nchini Marekani wenye lengo la kuleta mabadiliko chanya katika Sekta ya Elimu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (kulia) akizungumza na Mkuu wa Idara ya Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) ofisi ya Tanzania, Dkt.Daniel Baheta (Kushoto). Dkt.Baheta alimtembelea Waziri Mkenda ofisini kwake jijini Dodoma kujadiliana mambo mbalimbali yahusuyo mageuzi ya elimu nchini. (Picha na Wizara ya Elimu).

Katika kikao hicho Waziri Mkenda aliwahakikishia mashirika hayo ushirikiano katika kuleta mageuzi ya elimu nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news