Waziri Ummy amwakilisha Rais Samia kikao cha Kimataifa cha UVIKO-19 kwa njia ya mtandao

NA MWANDISHI-WAF

WAZIRI wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu leo amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kikao cha pili cha 'Global Covid-19' kwa njia ya mtandao ulioandaliwa za Serikali ya Belize, Ujerumani, Indoneaia, Senegal na Marekani.
Katika kikao hicho Waziri Ummy amesema hadi kufikia Mei 9, 2022 jumla ya dozi 7,713,526 za chanjo ya UVIKO-19 zimetolewa nchi nzima na watu wapatao 4,110,884 sawa na asilimia 13.37 wamepata chanjo hiyo ambayo makadirio yake ni kuchanja watanzania wapatao 30,740,928.

Waziri Ummy amesema hadi sasa Tanzania imeshapokea dozi 11,232,374 kutoka COVAX facility pamoja na washirika wengine.

Vilevile Waziri Ummy ameeleza katika kikao hicho kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha wananchi wanapata Chanjo dhidi ya UVIKO-19 ikiwemo kutoa elimu ya umuhimu wa chanjo kwa kuwa hatujui wimbi jingine la Kirusi litakuaje.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news