Dkt.Jingu asisitiza bidii,maadili,ubunifu na uwajibikaji kwa watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu-SBU

NA MWANDISHI WETU

WATUMISHI wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wameaswa kuendelea kufuata maadili ya utumishi umma kwa kufanya kazi vizuri na kuwa wabunifu katika utendaji wa kazi, ili kuepuka kufanya kazi kwa mazoea.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dkt. John Jingu pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Charles na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Bw. Kaspar Mmuya wakifutilia kwa umakini semina ya wafanyakazi kwa watumishi wa wizara hiyo iliyofanyika ukumbi wa tume ya Uchaguzi Dodoma.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu, Dkt. John Jingu wakati wa semina kwa wafanyakazi wa Ofisi hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Uchaguzi Mjini Dodoma katika Kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa umma; yenye kauli mbiu “Nafasi ya Mapinduzi ya Nne kwa Viwanda katika Masuala mapya yanayojitokeza kuhusu utoaji wa huduma na urejeshwaji wakati na baada ya janga la Corona.”
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dkt. John Jingu akizungumza katika semina ya watumishi wa Ofisi hiyo Uliofanyika katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa umma.

“Serikali kupitia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imeshatimiza wajibu wake kwa kuhakikisha maslahi ya wafanyakazi; marupupu, vitendea kazi vinapatikana, jukumu letu ni kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha kwamba wananchi wanafurahia huduma wanayopatiwa na Serikali," alisema Dkt.Jingu.
Alifafanua vikao hivi ni muhimu na vinapaswa kufanyika mara kwa mara ili kuweza kujua mipaka ya kiutendaji wa kazi iko wapi. "Lazima tufanye kazi kama timu kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa".
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakisikiliza na kufuatilia kwa umakini,Dkt. Revocatus Baltazary Ofisi ya Mganga Mkuu Jiji la Dodoma (hayupo pichani) katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma.(Picha na OWM).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news