Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Juni 24,2022

WIZARA YA MAJI INAVYOMNG’ARISHA RAIS SAMIA

UPATIKANAJI wa huduma ya majisafi na salama ni miongoni mwa masuala yanayopewa kipaumbele kikubwa na cha kipekee na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aprili 22, 2022 wakati akihutubia Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, Mhe. Samia aliweka bayana dhamira ya Serikali katika kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya ukosefu wa huduma ya majisafi na salama.

Mhe. Samia alisema miradi mingi imekuwa ikitekelezwa kwa kutumia fedha nyingi, lakini baada ya muda mfupi maji hayapatikani na hivyo akaelekeza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa miradi ya maji ili kuleta tija inayokusudiwa.

“Katika miaka hii mitano, tutaweka mkazo mkubwa katika kuimarisha usimamizi kwenye utekelezaji wa miradi ya maji. Lengo letu ni kufikia azma ya kufikisha huduma ya maji kwa wananchi kwa asilimia 95 mijini na asilimia 85 vijiji ifikapo mwaka 2025,” alisema Mhe. Samia.

Azma na dhamira ya dhati ya Mhe. Rais Samia ya kumtua mwanamke ndoo ya maji kichwani inatekelezwa vyema na Wizara ya Maji ambayo imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali kuhakikisha Watanzania wanafikiwa na huduma hiyo ili kutimiza ndoto ya Mhe. Rais Samia ya kuhakikisha huduma ya majisafi na salama inawafikia wananchi wengi.

Ni dhahiri kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi mitatu tangu Mhe. Rais Samia alipoingia madarakani Machi 19, 2021, mafanikio mengi ya kiuchumi na kijamii yameshuhudiwa katika uongozi wake...........

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news