Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2021

NA DIRAMAKINI

KWA mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mwaka 2021, thamani halisi ya Pato la Taifa ilifikia shilingi milioni 135,517,812.70 ikilinganishwa na shilingi milioni 129,130,182.02 mwaka 2020, sawa na ukuaji wa asilimia 4.9 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 4.8 mwaka 2020. 

Kuongezeka kwa kiwango cha ukuaji kulitokana na uwekezaji wa kimkakati hususani katika miundombinu ya nishati, maji, afya, elimu, ujenzi wa barabara, reli na viwanja vya ndege; kuongezeka kwa uzalishaji wa madini hususani dhahabu na makaa ya mawe; na kuongezeka kwa mikopo katika sekta binafsi ambayo imechochea shughuli za kiuchumi. 

Sekta zilizokua kwa viwango vikubwa katika kipindi husika ni pamoja na: sanaa na burudani (asilimia 19.4); umeme (asilimia 10.0); madini (asilimia 9.6); na habari za mawasiliano (asilimia 9.1). 

Sekta za malazi na huduma ya chakula pamoja na sanaa na burudani ambazo mwaka 2020 ziliathiriwa kwa kiasi kikubwa na UVIKO - 19 zilianza kukua kwa viwango chanya mwaka 2021 kufuatia kuimarika kwa huduma za utalii ambazo zina mchango mkubwa katika sekta hizo. 
Kielelezo Na. 1.1: Ukuaji wa Pato la Taifa kwa Shughuli za Kiuchumi (asilimia)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news