Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) latoa tamko manyanyaso ya wauza magazeti Dar


"Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limesikitishwa na vitendo vilivyofanywa na askari wa Jiji la Dar es Salaam vya kuwanyanyasa na kuchukua meza za wauza magazeti wanaofanya shughuli zao maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

"Matukio haya ya uonevu kwa wauza magazeti yamethibitishwa kufanywa na mgambo wa Jiji dhidi ya wauza magazeti bila kuwapo sababu zilizoainishwa kufanya hivyo. 

"Ikumbukwe kwamba Oktoba mwaka jana, serikali ilianza kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga) pembezoni mwa barabara za Jiji la Dar es Salaam, lakini wauza magazeti hawakuondolewa si kwa bahati, bali kwa mujibu wa Sheria ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya Mwaka 2014 nyongeza ya 9(3) HSC 4902.90.00 inayotambua magazeti kuwa ni nyenzo ya elimu si biashara.

Sheria hii inafanana na sheria karibu zote za kodi ya mapato na VAT duniani kote na ndiyo maana katika miji yote duniani kuna meza za magazeti na vitabu katika kona za mitaa kwa ajili ya kuendeleza elimu na maarifa kwa watu wake; 


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news