Karsan awauma sikio wanahabari, akemea habari za uongo,potofu na chonganishi

NA SHEILA KATIKULA

WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kufuata kanuni na maadili ya kazi zao ili kuepuka malalamiko ya habari zisizokuwa na usahihi.


Hayo yamesemwa jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan kwenye mkutano wa kupitia na kuthibitisha kanuni za maadili ya uandishi wa habari za mtandaoni na vyombo vya kawaida.

Amesema kuwa, ni vema waandishi wa habari za mitandaoni kuzingatia maadili ya uandishi wa habari ili kuepuka kuandika habari za uongo, habari potofu na habari chonganishi.

Hata hivyo amewataka waandishi wa habari za mitandao ya kijamii kuwa mabalozi wazuri kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya UVIKO – 19 pamoja na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi Zuma la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, mwaka huu.
Kwa upande wake Afisa Programu wa UTPC, Victor Maleko ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa Ushirikiano kati ya UTPC na International Media Support (IMS) amesema, ni vema waandishi wa habari za mitandao ya kijamii kufuata kanuni na maadili ya Uandishi wa Habari za mtandaoni ili waweze kuandika habari zenye usahihi.

"UTPC kwa kushirikina na IMS ilianza mchakato wa kutengeneza kanuni za maadili ya uandishi wa habari kwani maoni yalichukuliwa kwenye klabu nane za waandishi wa habari zikiwemo Dodoma, Mwanza,Zanzibar,Mtwara,Kigoma,"amesema Maleko.
Mwezeshaji ambaye ameshiriki Kutengeneza kanuni za maadili ya Uandishi wa Habari za mtandaoni, Pili Mtambalike amewataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, Chausiku Said na Maridhia Ngemela wamesema, watakuwa mabalozi wa kuhamasisha waandishi wa habari kufuata maadili na kanuni za uandishi wa habari ili kuepusha kuandika habari za kupotosha jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news