Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaanza ujenzi Mji wa Serikali Dodoma

NA PRISCA ULOMI-OWMS 

WAWAKILISHI wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) wakiongozwa na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende wameshuhudia makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali lenye ukubwa wa mita za mraba 17,342. 
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende (aliyesimama katikati) akiwa na wawakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT na TBA pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya hafla fupi ya kukabidhi eneo la ujenzi wa jengo la makao makuu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali lililopo Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma. 

Makabidhiano hayo yamefanyika Juni 18, 2022 kwenye Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma baina ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye ni Mshauri Elekezi aliyewakilishwa na Msanifu Majengo Weja Ng’olo na Kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT ambae ni Mkandarasi iliyowakilishwa na Mkadiriaji Majenzi, Jacob Ghati.

Akikabidhi eneo hilo, Mwakilishi wa TBA, Ng’olo ameeleza kuwa jengo la Ofisi linalotarajiwa kujengwa ni la kisasa na ni miongoni mwa majengo yenye muonekano mzuri katika Mji wa Serikali Mtumba. 
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende (aliyesimama katikati) akiwa na wawakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT na TBA pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya hafla fupi ya kukabidhi eneo la ujenzi wa jengo la makao makuu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali lililopo Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma. 

Jengo hilo litakuwa na miundombinu mbalimbali ikiwemo vyumba vya Ofisi 127, maegesho ya magari 111, maktaba, kumbi 2 za mikutano zenye nafasi 108 kila mmoja, kumbi 2 za kutolea mafunzo zenye nafasi 42 kila mmoja, maabara ya kompyuta, vyumba vidogo 10 vya mikutano na chumba cha akina mama wanyonyeshao. Ujenzi wa jengo hilo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi kumi na nane (18).
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende (wa tatu kulia) akipata maelezo kutoka kwa mwakilishi wa TBA, Msanifu Majengo Weja Ng’olo na Mwakilishi wa SUMA JKT, Jacob Gati (wa kwanza kushoto) wakati wa makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwenye Mji wa Serikali Mtumba Dodoma. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkandarasi, Gati amesema kuwa wako tayari kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa mujibu wa mkataba na kwa kushirikiana na Mshauri Elekezi (TBA) na Mshitiri (OWMS). 
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende (wa pili kulia) akishuhudia wawakilishi wa TBA wakiwaonesha mipaka wawakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bw. James Kibamba na kulia ni Mkurugenzi wa Mipango, Dkt. Abdul Mussa. 

Kwa upande wake, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Luhende amewatakia Mkandarasi na Mshauri Elekezi utekelezaji mwema wa majukumu yao kwa mujibu wa mkataba na kwa kuzingatia weledi. Pia amewahakikishia kuwa Ofisi ya Wakili Mkuu Serikali itawapa ushirikiano unaostahili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news