RC Kunenge akagua mradi wa kiwanda cha Sukari cha Lake Agro Investment Ltd Rufiji

NA ROTARY HAULE

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kilimo cha miwa na kiwanda cha Sukari cha Lake Agro Investment Ltd) kilichopo Utete wilayani Rufiji.
Kunenge amefanya ziara maalum ya kutembelea na kukagua mradi ambapo pamoja na mambo mengine ameeleza namna ambavyo mradi huo utakavyowanufaisha wananchi wa Rufiji, mkoa na Taifa kwa ujumla.

Akiwa katika eneo la mradi huo Kunenge amesema kuwa wawekezaji hao wapo kwenye matayarisho ya uwekezaji na kuwa eneo linalotarajiwa kuwekezwa lina ukubwa wa hekta 15 na uzalishaji wake utakuwa tani laki moja Sukari.

"Wawekezaji hawa ni wawekezaji makini na mpaka sasa tayari wamejenga njia ya umeme iliyogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 100 pamoja barabara za kufika eneo la mradi inajengwa,"ameeleza Kunenge

Kunenge, amesema kuwa matarajio ya Serikali juu ya mradi huo ni kupata kodi pamoja na kutoa ajira zaidi ya watu 18,000 zikiwemo za muda mrefu na mfupi sambamba na wananchi kupata utaalamu wa teknolojia mpya ya kilimo.
"Mradi huu utakuwa na faida kubwa kwetu sisi WanaRufiji,Mkoa na Taifa na kutokana na umuhimu huo tumekubaliana na uongozi wa Halmashauri kuhakikisha tunalipima eneo lote linalozunguka mradi ili kuondoa migogoro ya ardhi inayotokana na mipaka,"amesema Kunenge

Aidha , Kunenge amesema kuwa mradi huo utawanufaisha wakulima wengine wa nje(Outgrowers) kwa kupata msaada wa kitaalamu kutoka kwa wawekezaji hao ili kusudi kiwanda hicho kipate miwa ya kutosha.

"Kuwepo kwa kiwanda hiki ni juhudi za Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kufungua fursa kwa wawekezaji ,kwahiyo nasisi wasaidizi wake tupo tayari kukisimamia kiwanda hiki ili kiweze kuwa na matokeo chanya,"amesema Kunenge

Kunenge , amewataka wananchi wanaozunguka kiwanda hicho kujipanga kwa ajili ya kutumia fursa ya uwepo wa kiwanda hicho ili kusudi bidhaa zinazotakiwa kiwandani hapo zitokane pia na wananchi wenyewe.
Naye mwakilishi wa kampuni ya Lake Agro Investment Abubakar Nassor amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji hapa nchini.

Hata hivyo,Nassoro ametoa wito kwa Wananchi kuchangamkia fursa hiyo kwa kulima miwa kwa wingi na kuuza katika kiwanda hicho ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia kipato watakachopata katika kiwanda hicho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news