RC Mtaka asisitiza umuhimu wa sheria ndogo za mazingira

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka ameagiza Jiji la Dodoma kuharakisha sheria ndogo ndogo za mazingira ili kuweka hali ya usafi katikati ya jiji hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka (wa tatu kushoto) akipokea msaada wa vifaa vya kutunza taka kutoka kwa Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori vyenye nia ya kusaidia utunzaji wa mazingira katika jiji la Dodoma. Wengine kwenye picha ni Naibu Meya wa Jiji la Dodoma,Emmanuel Chibago, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Dkt.Fatma Mganga, Afisa Mkuu Rasilimali watu,Emmanuel Akonaay na Mkuu wa Idara ya Huduma za serikali na Ofisi Ndogo za Makao Makuu Dodoma wa NMB,Vicky Bishubo.

Mtaka alitoa agizo hilo kwa Naibu Meya wa Jiji la Dodoma, Emmanuel Chibago wakati wa kupokea vifaa vya kuhifadhia taka vilivyotolewa na benki ya NMB ili kusaidia utunzaji wa mazingira.

"Siku ile tulipata aibu kubwa, niliamua kuandika kwa mkono wangu kuomba vifaa hivi kwa benki ya NMB na leo wameleta,sasa naagiza vikabidhiwe kwa maandishi ili kila mmoja awe na wajibu wa kutunza na kuvifanyia kazi," alisema Mtaka.

NMB wamekabidhi jumla ya mapipa 100 yenye thamani ya zaidi ya Sh20 milioni wakiahidi kuendeleza ushirikiano na mkoa ili kuweka mji katika hali ya usafi.
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori alisema makabidhiano ya vifaa hivyo ni mipango ya benki hiyo katika kurudisha sehemu ya faida kwa wananchi baada ya kodi ambapo mwaka huu wametenga Sh.bilioni 2.9 ikiwa na ongezeko la 41% ukilinganisha na Sh.bilioni 2.05 za mwaka jana.

Kimori alisema walipokea ombi la vifaa vya kutunzia taka (dusty been) 350 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa lakini kwa kuanza wametoa 100.

Awali Katibu Tawala wa mkoa Dkt.Fatuma Mganga alisema, baada ya makabidhiano hayo, sheria za usafi zitaanza kutekelezwa kwa mtu atakayetupa taka hovyo huku Dkt. Mganga akisema, awali ilikuwa ngumu kutekeleza sheria hiyo kwa sababu maeneo mengi hayakuwa na vifaa vya kuhifadhia taka hivyo kila mmoja alitupa kama anavyoona inafaa.
Mkuu a Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akiwa amebeba moja ya vifaa vya kuhifadhia taka vilivyotewa na Benki ya NMB yenye nia ya kusaidia utunzaji wa Mazingira katika jiji la Dodoma. NMB ilikabidhi vifaa 100 kwa ajili ya Mkoa wa Dodoma kwenye viwanja vya Nyerere square jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news