Waziri Balozi Mulamula ateta na ujumbe kutoka NABA na NORFUND

Mhe. Waziri Mulamula akipokelewa na viongozi wa Chama cha ushirikiano wa Wafanyabiashara kati ya Norway na Nchi za Afrika na Mfuko wa Maendeleo wa Norway.
Picha ya pamoja na viongozi wa NABA na NORFUND.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ametembelea ofisi za Makao Makuu ya Mfuko wa Maendeleo wa Norway (NORFUND) na kuzungumza na uongozi wa mfuko huo pamoja na uongozi wa Chama cha ushirikiano wa Wafanyabiashara kati ya Norway na Nchi za Afrika (NABA) tarehe 17 Juni 2022 jijini Oslo, Norway. Katika ziara yake nchini Norway Waziri Mulamula amekutana na taasisi hizo za maendeleo ili kuona namna ya kuboresha sekta za ushirikiano zilizopo kati ya Norway na Tanzania na kuleta manufaa kiuchumi kwa pande zote mbili.
Sehemu ya uongozi wa Chama cha ushirikiano wa Wafanyabiashara kati ya Norway na Nchi za Afrika na Mfuko wa Maendeleo wa Norway wakifatilia mazungumzo ambapo waneonesha nia ya kuongeza maeneo ya ushirikiano ili kuleta tija zaidi katika soko la kimataifa na kuboresha miundombinu wenzeshi.
Sehemu ya Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo, kutoka kushoto ni Bi. Tunsume Mwangolombe na wa pili kushoto ni Bw. Seif Kamtunda.
Mazungumzo yakiendelea, Kutoka kulia Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga na Afisa Mambo ya Nje Bi. Kisa Doris Mwaseba.
Picha ya pamoja Mhe. Waziri Mulamula na Mkurugenzi wa NABA, Bw. Eivind Fjeldstad (kulia) na Mkurugenzi wa NORFUND Bw. Tellef Thorleifsson (kushoto).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news