WAZIRI NDUMBARO AFAFANUA JINSI SERIKALI ILIVYOZINGATIA HAKI ZA BINADAMU KWA WAKAZI WA NGORONGORO WALIOHAMIA HANDENI KWA HIYARI

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali imezingatia vyema suala la Haki za Binadamu kwa wakazi waliokuwa wanaishi Ngorongoro kisha kuamua kuanza kuondoka kwa hiyari yao kuelekea Kijiji Cha Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo kwenye kikao na wadau wa Haki za Binadamu pamoja na Wakuu wa Mikoa ya Arusha na Tanga, Mhe. John Mongella na Mhe. Adam Malima tarehe 21 Juni, 2022.

"Serikali imezingatia vyema haki za binadamu, imewajengea nyumba wananchi walioamua kuhama kwa hiyari, imewapa maeneo yasiyopungua hekari 3 kila mmoja, imewasafirisha wao na mizigo yao na mifugo wanayomiliki, lakini pia Serikali imewalipa fidia,"amesema.

Waziri Ndumbaro alisema imekuwa ni muhimu wadau wa Haki za Binadamu kukutana na kujadili suala la Ngorongoro na Loliondo ili kuhakikisha haki za binadamu zinazingatiwa na kujibu hoja zisizo za kweli zinazosambaa kwa haraka katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Awali, Dkt. Ndumbaro alitoa wasilisho katika kikao na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali na taasisi za kimataifa, liloonesha jinsi Serikali inavyozingatia haki na malengo yake kuboresha hali ya watanzania wa maeneo ya Ngorongoro na Loliondo.

Waziri Ndumbaro alisema kwa upande wa Loliondo, Serikali imewapa wananchi zaidi ya asilimia 62 ya eneo la hifadhi ya Loliondo ili kukidhi mahitaji ya wakazi wa sasa na imebakiwa na kiasi cha Kilomita za mraba 1500 kutoka 4000 za awali.

Mawasilisho ya wataalam yameonesha umuhimu wa kuhifadhi maeneo ya Loliondo na Ngorongoro kutokana na sababu za kimazingira na Ikolojia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news