Al-Ahly yatwaa ubingwa Afrika,Pitso kupewa bonasi Bilioni 1.2/-

Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al-Ahly ya Misri wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa tisa baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wao wa Zamalek, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Zamalek ambao hawajatwaa ubingwa tangu walipovuliwa na Simba SC mwaka 2003 walipata bao kupitia kwa Amr Mohamed El Soleya.
  
Baada ya Al Ahly kutangulia kufunga bao.Walitumia nafasi yao vizuri kuanzia mwanzo, dakika nne baada ya mechi kuanza walipata kona ya kwanza kutokana na juhudi za winga wao matata, Hussein Ali Elshahat. Kutokana na kona hiyo, El Soleya alishambulia safu ya ulinzi ya Zamalek na kutia kimyani bao safi.
 
Katika mtanange huo wa Novemba 27, 2020 wakati wengi wakiamini kuwa mechi hiyo watashuhudia dakika zaidi ya 100,bao la dakika za mwisho la Mohamed Magdy liliipatia ushindi Al Ahly dhidi ya mahasimu wao wa Cairo Zamalek katika fainali hiyo.

Aidha, bao la Magdy la dakika ya 88 lilikamilisha mechi hiyo ya kusisimua ambayo timu yake ilikuwa kifua mbele mapema kupitia goli la Amr El Soleya, lakini likasawazishwa kabla ya muda wa mapumziko.
 
Kocha wa Al Ahly ambao ni mabingwa wa kihistoria ya Misri, Pitso Mosimane, ametwaa taji lake la pili la klabu Bingwa Afrika baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza 2015/2016 akiwa na Mamelodi Sundowns ya nyumbani Afrika Kusini.

Baada ya kuiwezesha Al Ahly kutwaa taji la tisa la Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na kukaa na ukame kwa miaka saba inatajwa kuwa, atapewa bonasi ya shilingi bilioni 1.2.

Aidha, Pitso anaingia katika rekodi ya kuwa kocha wa tatu aliyewahi kutwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili akiwa na timu mbili tofauti kwa sasa.
 
Mashindano ya mwaka 2020 yalicheleweshwa kutokana na janga la virusi vya Corona (Covid-19), huku hatua zilizochukuliwa kudhibiti kuenea kwa virusi ikilazimu finali ya kwanza ya klabu bingwa Afrika kati ya timu mbili kutoka nchi moja kuchezwa bila kuwa na mashabiki uwanjani.

Post a Comment

0 Comments