Maisha jela kwa kumlawiti mtoto

Mahakama  ya  Hakimu  mkazi  Mkoa  wa  Tabora  imemuhukumu, Meshack James (21) kifungo  cha  maisha jela ambaye anajishughulisha na kazi ya kusafirisha abiria kwa baiskeli mjini Tabora, anaripoti Mwandishi Diramakini.

James amehukumiwa  baada  ya  kukutwa na hatia ya  kumlawiti mtoto mwenye  umri  wa  miaka minne  ambaye  alipewa  kazi  na  wazazi  wa  mtoto  huyo  ya  kumpeleka  shule  na  kumrejesha  nyumbani mjini humo.

Imedaiwa  mahakamani  hapo  na  Wakili  upande  wa  Jamhuri,  Tito Mwakalinga  kuwa,  mshtakiwa  huyo alitenda  kosa  hilo  kinyume  na  kifungu  cha  154  Ibara  ndogo  ya  kwanza  na  ya  pili Julai 2, mwaka  huu alipokuwa  akimrudusha nyumbani  mtoto  huyo ambaye jina linahifadhiwa.

Katika  maelezo  hayo  yaliyowasilishwa  mahakamani  na  Wakili  huyo  katika  shauri  hilo  la  ukatili  dhidi  ya  mtoto  Namba  89/2020 likionesha madai  ya  kumlawiti mtoto  huyo na  kutolewa ushahidi na mashahidi  watano.

Miongoni mwao ni daktari  ambapo  Mahakama imejiridhisha  bila  shaka  kwamba  kijana huyo alimfanyia  ukatili  huo wa  kumlawiti  mtoto  huyo  wa  kiume akiwa nyumbani  kwake na  kisha  kumtelekeza  mtoto  nje. 

Aidha, Hakimu Mkazi  Mkoa  wa  Tabora, Jovin  Kato  ametoa hukumu hiyo akisema iwe  fundisho  kwa  watu  wengine  wenye  tabia  chafu  ambayo kimsingi  haikubaliki  katika  jamii  na  kwamba  inawadhalilisha  watoto kwa ujumla ndani na nje ya mkoa huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news