Polisi waanza uchunguzi Uganda

Polisi nchini Uganda imeanza kufanya uchunguzi wa ghasia za ukandamizaji dhidi ya waandamanaji wiki iliyopita ambazo zinadaiwa kusababisha vifo vya watu 45,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kwa mujibuwa Gazeti la Daily Monitor,Msemaji wa Polisi, Fred Enanga amesema uchunguzi huo unazingatia zaidi makosa yaliyosababisha uharibifu.


Wajumbe wa Umoja wa Ulaya tayari wametoa wito wa kufanywa uchunguzi huru zaidi, kutokana na vitendo vya polisi dhidi ya waandamanaji ili kuhakikisha sheria inafuata mkondo wake kwa walioathiriwa na kuepuka kutohukumiwa waliohusika na ukatili ambao ni lazima wachukuliwe hatua.

Wiki iliyopita polisi walionekana wakitumia nguvu na silaha wakati wakipambana na waandamanaji waliokuwa wanalalamika dhidi ya kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Robert Chagulani maarufu kama Bobi Wine ambaye pia ni mgombea urais.

Post a Comment

0 Comments