Waziri Chamuriho akagua ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho akishuka kutoka kwenye sehemu ya meli mpya ya MV Mwanza “Hapa Kazi Tu” inayojengwa juu ya Chelezo, baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wake, mkoani Mwanza. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho (mwenye suti ya mikono mifupi) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi-Uchukuzi, wakati walipokagua maendeleo ya ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza “Hapa kazi Tu” mkoani Mwanza
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi-Uchukuzi, wakimsikiliza Kaimu Mhandisi Mkuu Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Mhandisi Abel Gwanafyo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Meli mpya ya MV Mwanza “Hapa kazi Tu’ jijini Mwanza.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho akitoa maelekezo kwa Menejimenti ya Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) na wajumbe wa baraza la Wafanyakazi-Uchukuzi, baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Meli ya MV Mwanza “Hapa kazi TU”, mkoani Mwanza. 
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi-Uchukuzi na Kaimu Katibu Mkuu, Gabrieli Mlgire (wa tano kushoto mbelel) katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza, mara baada ya kukagua meli hiyo jijini Mwanza.

Post a Comment

0 Comments