Rais Dkt. Mwinyi amteua Dkt. Ali Ahmed Uki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji la Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Dk. Ali Ahmed Uki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC), anaripoti Mwandishi Diramakini, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said, Rais Dk. Mwinyi amemteua Mwenyekiti huyo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 8 (1) (a) cha Sheria ya Shirika la Utangazaji Namba 4 ya mwaka 2013.
Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo, imeeleza kuwa, uteuzi huo umeanza tarehe 05 Februari, 2021.

Post a Comment

0 Comments