CHADEMA wataka Katiba mpya

NA MWANDISHI DIRAMAKINI, Arusha

"Hatukwenda kwenye siasa kutafuta ruzuku, tumeingia kwenye siasa kutafuta uongozi wa haki.Tutaidai katiba na tutaongoza mapambano ya kudai. Tuimarishe chama chetu, kama tuna chama legelege, hatuwezi kuongoza mapambano hayo;
Hayo yamesemwa leo Mei 27, 2021 na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe jijini Arusha katika mkutano uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali na wajumbe 214.

Pia Mheshimiwa, Freeman Mbowe amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu kurejesha mchakato wa Katiba mpya kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Amesema, ni vyema wanachama wa chama hicho wakaendelea kumuombea Rais Samia ili arejeshe mchakato wa Katiba na utengamano wa vyama vya siasa nchini.

Mheshimiwa Mbowe amesema, hawatashiriki uchaguzi wowote hadi katiba mpya iundwe ili kila mmoja aweze kula keki ya Taifa na kuishi kama ndugu.

"Tunataka tuwe watu wakuunganisha Taifa tukafanye ushindani na kurejesha tabasamu la Watanzania na hatutegemei na sisi tukaibe kura hivyo tunawapa nafasi ya kujitafakari Tume ya Uchaguzi kwani waliona uonevu wa viwango kwa miaka mitano,"amesema Mbowe.

Mheshimiwa Mbowe amesema, wamezindua Chadema digital ambao utakuwa mpango mahususi wa kukishusha chama hicho zaidi hadi kwenye mioyo ya wananchi wa kawaida hasa baada ya maumivu waliyopata katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2020 nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news