HABARI KATIKA PICHA: Ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi wa KADCO leo Mei 10, 2021

Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma Mheshimiwa George Yambesi (wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uendelezaji Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO) Dkt. Natu Mwamba (wa pili kutoka kulia), Bw.Bambumbile Mwakyanjala (kulia) Mkurugenzi wa Miongozo, Uwezeshaji na Utafiti Tume ya Utumishi wa Umma na Bibi Christine Mwakatobe, (kushoto) Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KADCO wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa KADCO leo katika Ukumbi wa Mikutano wa KADCO-Kilimanjaro. (Picha na PSC).
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uendelezaji Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO) Dkt. Natu Mwamba (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo baada ya Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma Mhe. George Yambesi (wa pili kulia) kufungua mafunzo kwa watumishi wa KADCO yanayoratibiwa na Kitengo cha Miongozo, Uwezeshaji na Utafiti (Tume ya Utumishi wa Umma) wengine ni Bibi Christine Mwakatobe, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji KADCO na Bw. Bambumbile Mwakyanjala mratibu wa mafunzo haya yanayofanyika KADCO. (Picha na PSC).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KADCO, Bibi Christine Mwakatobe akimkaribisha Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma Mhe. George Yambesi (wa pili kushoto) katika ukumbi wa mikutano wa KADCO kufungua mafunzo ya watumishi wa KADCO yanayotolewa na Tume ya Utumishi wa Umma, wengine ni Bw. Bambumbile Mwakyanjala Mkurugenzi wa Miongozo, Uwezeshaji na Utafiti wa Tume, kulia ni Dkt. Natu Mwamba Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uendeshaji Uwanja wa Ndege wa Kilimajaro. (Picha na PSC).
WAWEZESHAJI wa mafunzo kwa watumishi wa KADCO (kutoka kulia) Bibi Celina Maongezi (Katibu Msaidizi) na Bw. Fanuel Mwakibete wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bibi Shani Kimanga Meneja Rasilimali Watu wa KADCO pamoja na Watumishi wa KADCO wakimsikiliza mgeni Rasmi Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma Mhe. George Yambesi (hayupo pichani) akifungua mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa KADCO- KIA. (Picha na PSC).

Post a Comment

0 Comments