Jaji Imani Aboud apendekezwa kugombea Urais wa Mahakama ya Afrika

Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kutoka Tanzania, Mhe. Jaji Imani Aboud amependekezwa kugombea Urais wa Mahakama hiyo.

Jaji Aboud amesema endapo atashinda katika nafasi hiyo na kuibuka mshindi itakuwa ni heshma kubwa kwa nchi na kwake mwenyewe kushika wadhifa mkubwa katika mahakama ya Afrika kuhusu masula ya haki za binadamu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kutoka Tanzania Mhe. Jaji Imani Aboud katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

“Endapo nitashinda katika nafasi hiyo na kuibuka mshindi itakuwa ni heshma kubwa kwa nchi yangu na kwangu mwenyewe kushika wadhifa mkubwa katika mahakama ya Afrika kuhusu masula ya haki za binadamu,” amesema Jaji Aboud

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema Tanzania inayo imani na Jaji Imani Aboud kwa kuwa ana uzoefu mkubwa katika masula ya kimahakama hivyo ushindi wake utakuwa ni sifa kwa Taifa na kwa wanawake kuendelea kushika nyadhifa kubwa sio Serikalini tu, bali kwenye taasisi na mashirika ya kimataifa.

“Watanzania tuna imani na Jaji Aboud kwa kuwa ana uzoefu mkubwa katika masula ya kimahakama hivyo ushindi wake utakuwa ni sifa kubwa kwa Taifa, tunamuombe kila la kheri,” amesema Balozi Mulamula

Majaji wengine wanaogombea nafasi hiyo ni kutoka katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Malawi na Cameroon ambapo Hayati Jaji Augustino Ramadhani ndie alikuwa Mtanzania wa mwisho kushika nafasi hiyo ya Urais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.

Post a Comment

0 Comments