Makamu wa Rais Dkt.Mpango atoa maagizo kwa kampuni zinazoagiza mbegu

Na Mwandishi Diramakini

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philp Mpango amezitaka kampuni zote zinazoagiza mbegu mbalimbali kutoka nje ya nchi kuzalisha hapa nchini ili kuwezesha uwekezaji wa ndani.
Pia wakuu wa taasisi za Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wametakiwa kujizatiti na kujipima katika kuzalisha mbegu bora zitakazoweza kutosheleza na kumfikia mkulima.

Ameyasema hayo leo Mei 27, 2021 kwenye Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Kumbukizi ya Kifo cha Hayati, Edward Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mjini Morogoro.

“Napenda nichukue nafasi hii kuzitaka kampuni zote ambazo zinaagiza mbegu kutoka nje kuzalisha mbegu hapa nchini na Wizara ya Kilimo ijipange kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa maelekezo haya na wasisubiri tuwaulize.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akifunga Wiki ya Maadhimisho ya 17 ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine leo Mei 27,2021 katika Kampasi ya Moringe Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Morogoro SUA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kituo cha kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu Dkt. Ladslaus Mnyome kuhusu Panya aliyepata mafunzo ya kufanya Utafiti wa kugundua Vimelea vya Kifua Kikuu pamoja na kugundua Mabomu yaliyotegwa Ardhini, alipotembelea Maonesho ya ufungaji Wiki ya Maadhimisho ya 17 ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine yaliyofanyika leo Mei 27,2021 katika Kampasi ya Moringe Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Morogoro SUA.

“Lakini taasisi zetu za magereza na Jeshi la Kujenga Taifa ni lazima zijizatiti katika kuzalisha mbegu bora na nawataka pia wakuu wa taasisi hizo wajipime utendaji wao wa kazi, tumechelewa sana hatuwezi kwenda kuwa nchi ya kipato cha kati cha juu kwa mwenendo wa tija ambayo tumeuelezea,"amesema Makamu wa Rais.

Dkt.Mpango amepongeza, jitihada zinazofanywa na chuo katika kuboresha teknolojia za kilimo uvuvi na mifugo na kuongeza kuwa pamoja na jitihada hizo bado tija siyo ya kuridhisha katika kuzalisha mazao ya kutosha.

“Napongeza jitihada zenu mlizozifanya katika kuonesha umahiri wenu katika kuboresha teknolojia za kilimo,uvuvi na mifugo, napenda nisisitize kuwa jitihada hizo bado hazitoshi.Hatuna budi sote kwa pamoja Serikali, Chuo Kikuu cha Kilimo, taasisi sekta binafsi na watu wengine tuangalie teknolojia hizi zinazovumbuliwa zinawafikiaje wakulima wa kawaida na kwa gharama nafuu,"amesema.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akipata maelezo kutoka kwa Mussa Gese Dotto Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Morogoro SUA ambae ni Mbunifu wa kutengeneza Gari Shamba, alipotembelea Maonesho ya ufungaji Wiki ya Maadhimisho ya 17 ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine yaliyofanyika leo Mei 27,2021 katika Kampasi ya Moringe Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Morogoro SUA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akitembelea Maonesho ya Wiki ya Maadhimisho ya 17 ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine yaliyofungwa leo Mei 27,2021 katika Kampasi ya Moringe Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Morogoro SUA.

Mkuu wa Chuo cha SUA, Jaji mstaafu Joseph Warioba akimkaribisha Makamu wa Rais amesema, lengo la kuanzishwa kwa chuo hicho ilikuwa kutaka kutoa elimu ya kilimo na mifugo na uvuvi kwa ajili ya kuongeza tija na kuwa na akiba ya kutosha.

Jaji Warioba amesema, hata hivyo bado malengo yaliyokusudiwa hayajafikia na kwamba inahitajika waendelee na kufanya utafiti vijijini kuhakikisha wanapata kilichokwamisha jitihada hizo.

Kwa upande wake,Makamu Mkuu wa Chuo cha SUA, Raphael Chibunda kwenye risala yake amesema, chuo hicho toka kianzishwe kimepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mitaala kutoka mitatu mwaka 1984 hadi 106 sasa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga Wiki ya Maadhimisho ya 17 ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine leo Mei 27,2021 katika Kampasi ya Moringe Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Morogoro SUA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akiagana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Morogoro SUA Mhe. Jaji Warioba baada ya kufunga Wiki ya Maadhimisho ya 17 ya Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine leo Mei 27,2021 katika Kampasi ya Moringe Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Morogoro SUA. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Prof.Chibunda amesema, kumekuwepo ongezeko la wanafunzi kutoka 400 mwaka 1984 hadi kufikia wanafunzi 14,581 na kuwafanya kupanua shughuli zao katika mikoa ya Katavi,Arusha,Njombe na Ruvuma.

Hata hivyo, mbali na mafanikio hayo, Prof. Chibunda amesema wanakabiliwa na changamoto ya upungufu na uchache wa miundombinu ya kufundishia na watumishi wa kada mbalimbali hususani wa taaluma katika chuo hicho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news