Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo awapa neno wanachama

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amewasisitiza wanachama wa chama hicho kuendelea kuifanyia kazi dhamira yao kwa lengo la kuwawezesha kufikia malengo.
Akizungumza na wanachama pamoja na viongozi wa majimbo wa ACT Wazalendo huko Shangani Mkokotoni, Kaskazini Unguja, katika ufunguzi wa ziara za kujitambulisha na kuzungumza na wanachama wa chama wa mkoa wa Kaskazini A (kichama), Mheshimiwa Othman alisema “ili kuifikisha Zanzibar sehemu inayostahiki, wanachama wana wajibu wa kuendeleza mshikamano katika kusimamia dhamira hiyo.

“Hilo ndilo jambo litakalosaidia Chama chetu kukuwa kwa siasa zake nchini,"alisema Mheshimiwa Othman.

Aidha, amewaomba viongozi wa chama katika mkoa huo kuendelea kukinadi chama cha ACT Wazalendo ili kuhakikisha chama hicho kinazidi kupiga hatua.

Mheshimiwa Othman amewahimiza wanachama hao kuendelea kuwa pamoja na viongozi wao na kuwahakilishia kuwa ataendelea kufanya kazi ili kukivusha chama hicho na kuyafikia malengo yake
Akitoa taarifa ya chama hicho kwa Mkoa wa Kaskazini A (kichama), Katibu wa Oganaizesheni Taifa, Ndg. Omar Ali Shehe, alisema viongozi wa mkoa wanaendelea kuhakikisha wanaongeza idadi ya wanachama wake ili kuiendeleza ngome ya chama katika mkoa huo.

Nao Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo (Zanzibar), Ndugu Juma Duni Haji, pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Ndg. Ismail Jussa, waliwahimiza wanachama katika mkoa huo kuendelea kumuenzi Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad kwa kufuata yale aliyoyahimiza ikiwemo umoja, mshikamano, ukweli pamoja na kuepukana na utengano, jambo ambalo litarudisha nyuma maendeleo ya chama chao.

Mheshimiwa Othman, alikamilisha ziara yake ya siku ya leo kwa kukutana na wanachama na viongozi wa mkoa wa Kaskazini B kichama, kikao kilichofanyika Bumbwini Mtendeni.

Kesho Mei 30, 2021 ziara itaendelea katika mikoa ya Magharib A na B (kichama).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news