Rais Dkt.Mwinyi aelekea Msumbiji kuhudhuria mkutano wa dharura SADC

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoka nchini leo kuelekea Maputo nchini Msumbiji kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), utakaofanyika nchini humo Mei 27,2021, ANARIPOTI MWANDISHI DIRAMAKINI (Zanzibar).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakisalimiana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama Zanzibar, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,wakati akielekea nchini Msumbiji kuhudhuria Mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika kesho jijini Maputo. (Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Viongozi wa Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akielekea Nchini Msumbiji kuhudhuria Mkoato wa SADC unaotarajiwa kufanyika kesho jijini Maputo Msumbiji. (Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akielekea nchini Msumbiji kuhudhuria Mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika kesho jijini Maputo.(Picha na Ikulu).

Akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi ameagwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdallah pamoja na viongozi wengine.

Mkutano huo wa nchi za SADC unaofanyika nchini Msumbuji unatarajia kujadili masuala ya hali ya ulinzi na usalama unawajumuisha viongozi wakuu kutoka nchi za Jumuiya (SADC) zikiwemo Msumbiji, Malawi, Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, na Zimbwabwe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news