Rais Dkt.Mwinyi ateta na Waziri Duddridge kutoka nchini Uingereza

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, James Duddridge na kumueleza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Nane katika kuhakikisha Zanzibar inapata maendeleo endelevu, ANARIPOTI MWANDISHI DIRAMAKINI.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo wakati alipofanya mazungumzo na Waziri anayehusika na masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza, James Duddridge katika Ikulu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshuhulika Masuala ya Afrika, Mhe. James Duddridge, alipofika Ikulu kwa mazungumzo akiongozana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe.David Concar, yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. (Picha zote na Ikulu).

Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi amemueleza Waziri huyo mipango na mikakati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane katika kukuza uchumi na kuendeleza ustawi wa wananchi wa Zanzibar.Rais Dk. Mwinyi alimueleza kiongozi huyo juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Nane katika kuendeleza ushirikiano na washirika wa Maendeleo pamoja na Taasisi za Kimaifa ambapo Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amemfahamisha kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuifanya Zanzibar kuwa kituo muhimu cha biashara cha ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa kuendeleza uchumi wa buluu ambao umejumuisha sekta ya utalii, uchimbaji wa mafuta na gesi uvuvi pamoja na sekta nyenginezo.Hivyo, Rais Dk. Mwinyi ameeleza haja kwa Waziri huyo kuwashajisha wawekezaji kutoka nchini Uingereza kuja Zanzibar kuzitumia fursa zilizopo za uekezaji katika sekta mbali mbali za maendeleo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshuhulikia masuala ya Afrika Mhe. James Duddridge, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya mlango wa Zanzibar mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddridge, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 12/5/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya mlango wa Zanzibar mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anauashuhulikia masuala ya Afrika Mhe. James Duddridge, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 12/5/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshuhulikia masuala ya Afrika Mhe. James Duddridge,baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshuhulikia masuala ya Afrika Mhe.James Duddridge wakitoka katika ukumbi baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshuhulikia masuala ya Afrika Mhe.James Duddridge wakitoka katika ukumbi baada ya kumaliza mazungumzoyao yaliofanyika Ikulu Jijini Zanzibar.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshuhulika Masuala ya Afrika. Mhe. James Duddridge, alipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafanya juhudi maalum za kuhakikisha kwamba kunakuwa na uwiano wa maendeleo baina ya kisiwa cha Unguja na kisiwa cha Pemba.Vile vile, kwa upande wa siasa, Rais Dk. Mwinyi alimueleza Waziri Duddridge kwamba juhudi kubwa zinafanywa na Serikali ya Awamu ya Nane katika kuhakiksiha kwamba Zanzibar inaendelea kuwa na amani, utulivu pamoja na mshikamano.

Rais Dkt. Mwinyi alieleza kwamba katika kuhakikisha maendeleo makubwa zaidi yanapatika hapa Zanzibar alihakikisha anashirikiana vyema na viongozi walioshiriki katika kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa ili kuhakikisha Zanzibar inabaki kuwa yenye amani.

Kwa upande wa maradhi ya COVID 19, ambayo yamekuwa yakiitesa dunia, Rais Dkt. Mwinyi alimueleza Waziri huyo hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuunda Kamati ya Wataalamu watakaoshauri juu ya mustakabali wa kukabiliana na janga hilo hapa nchini.

Alisisitiza kwamba kwa vile Zanzibar inaitegemea sana sekta ya Utalii, kutokana na kuwepo kwa maradhi ya COVID 19 kumepelekea kupungua kwa watalii wanaokuja kuitembelea Zanzibar na kusababisha kupungua kwa mapato.

Sambamba na hayo, Rais Dkt. Mwinyi alieleza haja kwa nchi hiyo kuunga mkono juhudi za Zanzibar katika kuunda mifumo maalum kwenye sekta za maendeleo zikiwemo sekta za afya na elimu.

Nae Waziri wa Uingereza anaeshughulikia masuala ya Afrika James Duddridge alieleza juhudi zilizochukuliwa katika kuhakikisha Serikali yake inaendelea kuziunga mkono nchi za Afrika.Katika kuhakikisha hilo linapata mafanikio makubwa alisema kuwa Serikali yake imetenga bajeti maalum katika kuzisaidia nchi za Afrika.

Aidha, Waziri Duddrigdge alieleza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Uingereza na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Zanzibar na kuahidi kuuendeleza.Waziri huyo alimuhakikishia Rais Dk. Mwinyi kwamba nchi yake itaiunga mkono Zanzibar katika kufikia malengo iliyojiwekea katika kujiletea maendeleo.

Alipongeza hatua za Rais Dkt. Mwinyi za kusimamia vyema Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuwaunganisha wananchi hali ambayo itaendeleza amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi wa Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments