Rais Dkt.Mwinyi, Waziri Mkuu waongoza sala ya Eid El Fitry


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Viongozi wa Serikali baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid El Fitry iliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar, leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi wa Serikali, Dini na Wananchi wa Zanzibar katika Sala ya Eid El Fitry, ikisalishwa na Sheikh Rashid Salim Dau, katika viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar.
Waumini wa Kiislam wakijumuka katika Sala ya Eid El Fitry iliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Jijini Zanzibar.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir Ally katika Swala ya Eid iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 14, 2021.
Kadhi Mkuu, Sheikh Ali Muhiddini Mkoyogole akiongoza Swala ya Eid kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 14, 2021. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alishiriki katika Swala hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Swala ya Eid iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 14, 2021 (Picha na Ikulu).

Post a Comment

0 Comments