RC KUNENGE ASEMA HAKUNA MACHINGA ATAKAEONDOLEWA WALA KUBUGUDHIWA DAR ES SALAAM

NA MWANDISHI DIRAMAKINI (Dar es Salaam).

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Abubakar Kunenge amesema hakuna mfanyabiashara mdogomdogo maarufu kama Machinga atakaeondolewa katika Jiji hilo kama taarifa za uzushi kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii zinavyodai ambapo amawataka wananchi kupuuzia taarifa hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge.

RC Kunenge amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa wamachinga kwenye mkoa huo hivyo amewataka waendelee kufanya biashara zao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu. TIZAMA LIVE CHINI

Aidha RC Kunenge amewataka machinga wasijenge kwenye mapito ya watembea kwa miguu Wala Barabarani kwani kwa kufanya hivyo wanahatarisha usalama wao na Vyombo vya Moto.

Pamoja na hayo RC Kunenge ametoa angalizo kwa wafanyabiashara wenye utaratibu wa kubeba mitungi ya gesi na majiko yanayowaka na kukatizanayo katikati ya watu na vyombo vya moto jambo ambalo ni hatari kwa kiusamama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news