TARI yagundua aina 26 za mihogo yenye mavuno mengi

Daktari Esther Andrew Masumba, mgunduzi wa mbegu bora za Muhogo ambaye pia ni Mratibu wa Utafiti wa Mazao ya Mizizi nchini chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania, akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mheshimiwa Abubakar Kunenge kuhusu baadhi ya mafanikio ya Utafiti wa Muhogo nchini, ikiwemo Ungunduzi wa aina 26 bora za Muhogo zenye mavuno zaidi ya tani 20 kwa hekta moja ikiwemo aina ya Pwani ambayo ina wastani wa Uzalishaji wa tani 50.8 kwa hekta.

Pia, mafanikio mengine ni kushiriki katika uundwaji wa mfumo rasmi wa mbegu za Muhogo, ili kudhibiti Uzalishaji wa mbegu bora, safi na salama kwa ajili ya usambazaji kwa mkulima.

Aidha, daktari Masumba aliongezea kwa kusema kuwa, changamoto kuu zinazoathiri tija ya Muhogo nchini ni kuwepo kwa Magonjwa mawili makuu, Batobato na Michirizi ya Kahawia.

Hivyo, pamoja na tafiti nyingine, Taasisi imefanikiwa kubaini mbinu za kudhibiti Nzi Weupe ambao ni wasambazaji wa Magonjwa hayo ambayo yana uwezo wa kupunguza tija ya Muhogo kati ya asilimia 80 hadi 100 kwa kutumia viuatilifu vilivyoyhibitishwa. (PICHA ZOTE NA JUNIOR MWEMEZI-AFISA HABARI WA TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO NCHINI-TARI).

Post a Comment

0 Comments