UONGOZI WA DIRAMAKINI WATOA UJUMBE MAALUM WA EID AL-FITR


Uongozi wa Kampuni ya Diramakini Business Limited ambao ni wamiliki wa www.diramakini.co.tz umewatakiwa Waislamu wote ndani na nje ya Tanzania Sikukuu njema ya Eid al Fitr. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ameeleza kuwa, hii ni siku muhimu sana katika kalenda ya Kiislamu ambayo husherekewa siku mbili, kuhitimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao hudumu kwa mwezi mmoja.

Taarifa hiyo imeelezea kuwa, umuhimu wake si kwa Waislamu pekee bali kwa watu wote kwani, Eid al-Fitr inaadhimishwa kama sherehe ya umma ili kujenga maana zaidi kwa jamii na kuunganisha makundi mbalimbali.

"Kwa msingi huo basi, Diramakini Business Limited inachukua nafasi hii kuwaomba watu wote kusherehekea kwa amani, upendo na mshikamano na kubwa zaidi kila mmoja achukue tahadhari dhidi ya maambukizo ya virusi vya ugonjwa wa Corona (COVID-19), huu ni ugonjwa ambao unaendelea kuisumbua Dunia, hivyo kila mmoja wetu azingatie kanuni za afya ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka, kutumia vitakasa mikono, kuepuka misongamano na kuzingatia uvaaji wa barakoa.

"Mbali na hayo, kila mmoja achukue tahadhari kwa watoto ili wasikabiliwe na vikwazo vya namna yoyote ile ikiwemo ajali wakiwa nyumbani au maeneo ya michezo, na kuhakikisha maeneo yetu ya makazi hatuondoki wote ili kuepuka changamoto ya kuibiwa mali zetu,"imeongeza taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments