Wadau wakutana kuhimiza kilimo cha mchicha

Wadau wa Jukwa la Ubunifu la Mchicha wamekutana jijini Dodoma, katika Ukumbi wa Chuo Cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) kwa lengo la kupata uelewa wa uzalishaji, usindikaji na matumizi ya zao la Mchicha. Jukwaa hilo lilifungiliwa na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Bi. Yustina Munishi. 

Mkutano huo ulishirikisha wakulima, wafanyabiashara hususan Wanawake na vijana.

Wakati wa uzinduzi wa Jukwaa hilo, washiriki walipata fursa ya kuzifahamu aina za mbegu za mchicha ambazo ni POLI, AKERI na NGURUMA. 

Wadau walifahamishwa kuwa Mchicha aina ya AKERI ni kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu pekee; aina ya NGURUMA ni kwa ajili ya uzalishaji wa majani pekee; wakati aina ya POLI ni kwa ajili ya uzalishaji wa majani na pia mbegu.

Jukwaa hili litasaidia kuhimiza kuongeza uzalishaji wa Mchicha na mbegu zake ili kuongeza kipato na lishe bora.(PICHA ZOTE NA JUNIOR MWEMEZI-AFISA HABARI WA TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO NCHINI-TARI).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news