ALIYOYASEMA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN WAKATI AKIZINDUA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU CHA MWANZA PRECIOUS METALS REFINERY TAREHE 13 JUNI, 2021 JIJINI MWANZA


Nimeingia ndani maeneo mbalimbali nimeona kiwanda kinavyofanya kazi vizuri. Nimeona miujiza, purity yake ni ya kiwango cha juu.

# Ni kiwanda kikubwa cha kisasa chenye uwezo wa kuzalisha kilo 480 kwa siku na kiwango cha juu kabisa cha Kimataifa cha asilimia 999.9.

# Napongeza ujenzi wa kiwanda hiki kwani kitaongeza mapato ya Serikali na ajira za moja kwa moja 120 na zisizo za moja kwa moja 400.

# Wasiwasi wangu ni upatikanaji wa malighafi, Serikali na Wizara mna kazi ya Kisera kuwezesha wachimbaji wachimbe.

# Ni ukweli usiopingika baada ya Mabadiliko ya Mwaka 2017 mengi yamefanyika katika Sekta ya Madini. Azma ya kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025 inakwenda kutimia.

#Sasa Benki Kuu ya Tanzania itaanza kununua dhahabu na kuweka amana ya Dhahabu ( Gold Reserve).

#Tunanataka Shughuli za uongezaji Thamani Madini tuzifanyie hapa hapa nchini. Anayetaka kuleta Dhahabu zake alete tutazisafisha kodi tutakata baadaye, tusikatae malighafi kutoka nje.

#Wachimbaji wa Dhahabu Kanda ya Ziwa fungeni mikanda kuchimba Dhahabu kwa kuwa kiwanda kinahitaji malighafi ya kutosha.

# Wizara fuatilieni watu waliochukua maeneo bila kuyaendeleza wapewe wengine waendeleze. Tuna kazi kubwa ya kujipandisha Uchumi wa Kati wa Juu na kubaki kwa muda.

#Wizara endeleeni kutenga maeneo yaliyofanywa utafiti kwa wachimbaji, wakiwezeshwa vifaa wanaweza. Eneo hili linaajiri watu wengi.

#Wakati umefika wa kui brand tena Tanzanite yetu kukifanya ya kipekee. Kuna haja ya kuwa na Mfumo wa kudhibiti Madini ya Tanzanite yanunuliwe na mwamvuli mmoja na imilikiwe na mwamvuli mmoja ili tuweze kuidhibiti. Mungu alitupa sisi tu dunia nzima.

#Tuna tatizo pale Liganga na Mchuchuma kuna mwekezaji amekaa na Leseni miaka 11 hajafanya chochote.Tatizo nusu ni yeye na nusu ni urasimu wetu wa Serikali.Wizara ondosheni vikwazo vyote kwa upande wa Serikali abaki yeye. Kamati ya Majadiliano kaeni naye mwambieni kuhusu Sheria zetu, akishindwa atafutwe mwingine.

# Serikali ilianzisha Masoko ya Madini na vituo vya ununuzi wa madini, hivi sasa tuna Masoko 39 na vituo vya ununuzi wa madini ,50.

# Tumetoa Leseni 4 za Smelter na Leseni ya Mgodi Mkubwa wa Nyanzaga, Mungu alitushushia utajiri wa kutosha.

# Wizara ikiimarishe Kituo Cha Jemolojia Tanzania (TGC) kinachotoa mafunzo ya Uongezaji Thamani Madini. Tuendelee Kujenga ujuzi kwa vijana watumie Madini kupata ajira utusaidie kupunguza tatizo la ajira. Kama Kuna changamoto ifanyieni kazi.

# Kazi iendelee, wachimbaji wadogo wasimamiwe wachimbe zaidi, wachimbaji wakubwa wachimbe, kazi iendelee.

ALIYOYASEMA WAZIRI WA MADINI DOTO BITEKO


# Kwa mara ya kwanza tangu Uhuru wa Nchi yetu tumeweka historia ya kuwa miongoni mwa nchi zinazosafisha madini yake.

# Mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria ya Madini Mwaka 2017 ndiyo yalitamka wazi kuwa Madini yote yaliyopo nchini katika maeneo mbalimbali yatakuwa chini ya usimamizi wa Rais ambaye ndiyo wewe msimamizi Mkuu wa Sekta ya Madini.

# Kiwanda hiki kitaongeza mapato ya Serikali kwa kuipatia shilingi bilioni 744 kwa Mwaka. Halmashauri shilingi bilioni 36 na STAMCO utapata shilingi bilioni 21.

#Tutatekeleza yote unayotuagiza, sauti yako bado tunaisikia na tunayafanyia kazi Maelekezo yote likiwemo lile la kuondoa urasimu kwenye Sekta ya Madini.

# Jumla ya Kampuni 34 zilituma maombi ya ujenzi wa kiwanda hiki na zote zilichujwa na hatimaye kupatikana Kampuni hii.

Kiwanda hiki cha Kusafisha Dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery ni moja ya Viwanda Vitatu vilivyojengwa nchini . Hiki ndiyo kiwanda kikubwa ambacho kitazalisha kilo 480 za Dhahabu kwa siku na baadaye zitaongezeka hadi kilo ,960. Kiwanda cha Dodoma kinasafisha kilo 30 kwa siku na Geita kilo 450 kwa siku. Haya ni mapinduzi makubwa sana.

# Huko nyuma tuliwahi kupendekeza Shirika la STAMICO lifutwe lakini sasa linafanya vizuri na linatekeleza miradi.

#Mchango wa Sekta ya umekuwa hadi kufikia asilimia 6.7 kutoka asilimia 4 3 Mwaka 2015. Kwa upande wa makusanyo tulipangiwa kukusanya shilingi bilioni 526 hadi kufikia Juni 1 tayari tumekusanya shilingi bilioni 544. Mwaka ujao wa fedha tumepangiwa kukusanya shilingi bilioni 650.

ALIYOYASEMA KATIBU MKUU WA MADINI PROF. SIMON MSANJILA

# Ujenzi wa Kiwanda hiki cha Kusafisha Dhahabu ni matokeo ya Mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria ya Madini Mwaka 2017 .

# Mradi huu una miradi midogo midogo mitatu ukihusisha ujenzi wa miundombinu na mitsmbo na majengo ambapo kutakuwa na Soko la Madini, Mradi mwingine ni wa kuwasaidia wachimbaji wadogo mitaji na vifaa na wa tatu ni mradi wa kuuza na kununua Dhahabu.

# Ujenzi wa Kiwanda hiki ulianza mwezi Machi 2020 na ulikamilika mwezi Machi ,2021 na uzalishaji wa kwanza ulianza mwezi Aprili, 2021.

ALIYOYASEMA MKURUGENZI MTENDAJI MIKUU WA KIWANDA CHA MWANZA PRECIOUS METALS REFINERY, ANAND MOHAN

# Ujenzi wa Kiwanda hiki ulikuwa wa safari ndefu kwangu lakini hatinaye leo tumefika hapa, Waziri wa Madini alikuwa bega kwa bega na sisi kuhakikisha tunafanikisha hili tunampongeza sana . Pia, tunamshukuru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella alitusaidia sana.

# Mhe. Rais tunaomba Serikali isiruhusu kusafirisha Dhahabu ghafi bali iongezwe thamani hapa nchini kwa kuwa kiwanda cha kufanya hivyo kipo.

# Mbali ya kiwanda hiki kuchangia mapato kwa Serikali lakini pia tutahakikisha kwamba uzalishaji unaendelea.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA MADINI NA STAMICO

Post a Comment

0 Comments